1  Nafsi yangu inachoka na maisha yangu; Sitajizuia na kuugua kwangu; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu. 
Job 7.11  1 Rois 19.4  Job 9.21  Nombres 11.15  Job 6.2-6.4  
 2  Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa; Nionyeshe sababu ya wewe kushindana nami. 
Job 9.29  Psaumes 143.2  Romains 8.1  Lamentations 5.16-5.17  Job 8.5-8.6  
 3  Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuyaangazia mashauri ya waovu? 
Esaïe 64.8  Job 14.15  Psaumes 138.8  Job 34.18-34.19  Job 8.20  
 4  Je! Wewe una macho ya kimwili, Au je! Waona kama aonavyo binadamu? 
1 Samuel 16.7  Luc 16.15  Job 9.32  Apocalypse 1.14  
 5  Je! Siku zako ni kama siku za mtu, Au je! Miaka yako ni kama siku za mtu, 
2 Pierre 3.8  Job 36.26  Psaumes 102.12  Hébreux 1.12  Psaumes 102.24-102.27  
 6  Hata ukauliza-uliza habari za uovu wangu, Na kuitafuta dhambi yangu, 
Job 14.16  Job 10.14-10.17  Jérémie 2.34  Sophonie 1.12  Jean 2.24-2.25  
 7  Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu; Wala hapana awezaye kuokoa na mkono wako? 
Deutéronome 32.39  Job 31.14  Jean 21.17  Job 42.7  2 Corinthiens 1.12  
 8  Mikono yako imeniumba na kunifinyanga; Nawe utageuka na kuniangamiza? 
Psaumes 119.73  Esaïe 43.7  Job 10.3  Jérémie 18.3-18.10  Genèse 6.6-6.7  
 9  Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena? 
Genèse 2.7  Esaïe 64.8  Genèse 3.19  Ecclésiaste 12.7  Jérémie 18.6  
 10  Je! Wewe hukunimimina kama maziwa, Na kunigandisha mfano wa jibini? 
Psaumes 139.14-139.16  
 11  Umenivika ngozi na nyama, Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa. 
2 Corinthiens 5.2-5.3  Ezéchiel 37.4-37.8  Job 40.17-40.18  Ephésiens 4.16  
 12  Umenijazi uhai na upendeleo, Na maangalizi yako yameilinda roho yangu. 
Matthieu 6.25  Actes 17.28  Job 33.4  Actes 17.25  Genèse 19.19  
 13  Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako; Najua kuwa haya yamo nafsini mwako; 
Job 23.13  Ecclésiaste 8.6-8.7  Romains 11.33  Ephésiens 3.11  Esaïe 45.7  
 14  Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia, Wala hutaniachilia na uovu wangu. 
Job 7.21  Psaumes 130.3  Job 13.26-13.27  Job 9.28  Psaumes 139.1  
 15  Mimi nikiwa mbaya, ole wangu! Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu; Mimi nimejaa aibu Na kuyaangalia mateso yangu. 
Esaïe 3.11  Job 9.15  Job 10.7  Job 9.20-9.21  Psaumes 25.18  
 16  Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba; Tena wajionyesha kwangu kuwa wa ajabu. 
Esaïe 38.13  Lamentations 3.10  Job 5.9  Osée 13.7-13.8  Deutéronome 28.59  
 17  Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu, Na kasirani yako waiongeza juu yangu; Jeshi kwa jeshi juu yangu. 
Job 16.8  Ruth 1.21  Psaumes 55.19  Sophonie 1.12  Jérémie 48.11  
 18  Kwa nini basi kunitoa tumboni? Ningekata roho, lisinione jicho lo lote. 
Jérémie 20.14-20.18  Job 3.10-3.11  Matthieu 26.24  Job 14.10  Job 11.20  
 19  Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo; Ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni. 
Psaumes 58.8  
 20  Je! Siku zangu si chache? Acha basi, Usinisumbue, nipate ngaa kutuzwa moyo kidogo. 
Job 14.1  Psaumes 39.13  Job 9.25-9.26  Job 13.21  Psaumes 39.5  
 21  Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena, Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu; 
2 Samuel 12.23  Job 3.5  Job 16.22  Psaumes 23.4  Job 14.10-14.14  
 22  Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo; Ni nchi ya giza tupu, isiyo na matengezo ya mambo yo yote, Nchi ambayo nuru yake ni kama giza. 
Psaumes 23.4  Psaumes 44.19  Jérémie 2.6  Job 38.17  Jérémie 13.16