Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Chroniques 28.20
Bible en Swahili de l’est


1 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; wala hakufanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, kama Daudi babaye;1 Chroniques 3.13 Esaïe 1.1 Esaïe 7.1-7.12 2 Rois 16.1-16.20 Matthieu 1.9
2 bali akaziendea njia za wafalme wa Israeli, akawafanyizia mabaali sanamu za kusubu.Exode 34.17 Juges 2.11 Osée 2.13 Juges 2.13 Lévitique 19.4
3 Tena akafukiza uvumba katika bonde la mwana wa Hinomu, akawateketeza wanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli.2 Chroniques 33.2 2 Chroniques 33.6 Lévitique 18.21 2 Rois 23.10 Josué 15.8
4 Akatoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu, na vilimani, na chini ya kila mti wenye majani mabichi.Lévitique 26.30 2 Rois 16.4 Deutéronome 12.2-12.3
5 Kwa hiyo Bwana, Mungu wake, akamtia mkononi mwa mfalme wa Shamu; wakampiga, wakachukua wa watu wake wafungwa wengi sana, wakawaleta Dameski. Tena akatiwa mkononi mwa mfalme wa Israeli, aliyempiga mapigo makuu.Esaïe 7.1 2 Rois 16.5-16.6 2 Chroniques 24.24 Exode 20.2-20.3 2 Chroniques 36.5
6 Kwa kuwa Peka mwana wa Remalia akawaua katika Yuda siku moja watu mia na ishirini elfu, mashujaa wote; kwa sababu walikuwa wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao.2 Rois 15.27 Esaïe 9.21 Deutéronome 29.24-29.26 2 Rois 16.5 Esaïe 7.9
7 Naye Zikri, mtu hodari wa Efraimu, akawaua Maaseya mwana wa mfalme, na Azrikamu mkuu wa nyumba, na Elkana, aliyekuwa wa pili wake mfalme.Esther 10.3 Genèse 43.12 Genèse 43.15 Genèse 41.43
8 Wana wa Israeli wakachukua wa ndugu zao wafungwa mia mbili elfu, wanawake, na wana, na binti, pia wakachukua kwao nyara nyingi, wakazileta nyara Samaria.2 Chroniques 11.4 Deutéronome 28.25 Deutéronome 28.41 Actes 7.26 Actes 13.26
9 Lakini kulikuwako huko nabii wa Bwana, jina lake aliitwa Odedi; akatoka kuwalaki jeshi waliokuja Samaria, akawaambia, Angalieni, kwa kuwa Bwana, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, yeye amewatia mikononi mwenu, nanyi mmewaua kwa ghadhabu iliyofikia mbinguni.Esdras 9.6 Esaïe 47.6 Apocalypse 18.5 Zacharie 1.15 Jérémie 15.17-15.18
10 Na sasa mwanuia kuwatawala wana wa Yuda na Yerusalemu, wawe kwenu watumwa na wajakazi; lakini ninyi nanyi je! Hamna hatia zenu wenyewe juu ya Bwana, Mungu wenu?Lévitique 25.39-25.46 Jérémie 25.29 1 Pierre 4.17-4.18 Romains 12.20-12.21 Matthieu 7.2-7.4
11 Haya, nisikieni mimi basi, mwarudishe wafungwa, mliowachukua mateka wa ndugu zenu; kwa maana ghadhabu ya Bwana iliyo kali i juu yenu.Jacques 2.13 Matthieu 5.7 Hébreux 13.1-13.3 Matthieu 7.2 Esdras 10.14
12 Ndipo wakaondoka juu ya hao waliotoka vitani baadhi ya wakuu wa wana wa Efraimu, Azaria, mwana wa Yohanani, na Berekia mwana wa Meshilemothi, na Yehizkia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai,Jérémie 26.6 1 Chroniques 28.1
13 wakawaambia, Hamtawaleta wafungwa humo; kwa sababu mnayanuia yatakayotutia hatiani mbele za Bwana, kuongeza dhambi zetu, na hatia yetu; maana hatia yetu ni kubwa, na ghadhabu kali ipo juu ya Israeli.Josué 22.17-22.18 Nombres 32.14 Matthieu 23.32 Matthieu 23.35 Romains 2.5
14 Basi watu wenye silaha wakawaacha wafungwa na nyara mbele ya wakuu na kusanyiko lote. 15 Wakaondoka wale watu waliotajwa majina yao, wakawatwaa wafungwa, wakawavika kwa zile nyara wote wao waliokuwa uchi, wakawapa mavazi na viatu, wakawalisha, wakawanywesha, wakawatia mafuta, wakawapandisha waliokuwa dhaifu miongoni mwao juu ya punda wakawaleta Yeriko, mji wa mitende, kwa ndugu zao; kisha wakarudi Samaria.Deutéronome 34.3 2 Rois 6.22 Proverbes 25.21-25.22 Juges 1.16 Luc 8.27
16 Wakati ule mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa mfalme wa Ashuru ili amsaidie.Esaïe 7.17 2 Rois 16.5-16.7 Esaïe 7.1-7.9
17 Kwa kuwa Waedomi walikuwa wamekuja tena, na kuwapiga Yuda, na kuwachukua wafungwa.Abdias 1.10 Abdias 1.13-1.14 Lévitique 26.18 2 Chroniques 25.11-25.12
18 Wafilisti pia walikuwa wameingia miji ya Shefela, na ya Negebu ya Yuda, nao wameutwaa Beth-shemeshi, na Ayaloni, na Gederothi, na Soko pamoja na miji yake, na Timna pamoja na miji yake, na Gimzo pia na miji yake; wakakaa humo.Ezéchiel 16.57 Ezéchiel 16.27 Josué 15.10 Juges 14.1 Josué 15.48
19 Kwa maana Bwana aliinamisha Yuda kwa ajili ya Ahazi mfalme wa Israeli; kwa kuwa yeye aliwafanyia Yuda aibu, na kumwasi Bwana mno.2 Chroniques 21.2 Proverbes 29.23 Exode 32.25 Genèse 3.7 Michée 6.16
20 Na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru akamjia, akamfadhaisha, asimtie nguvu kwa lo lote.2 Rois 15.29 Esaïe 30.16 1 Chroniques 5.26 Esaïe 30.3 2 Rois 17.5
21 Kwa maana Ahazi alitwaa sehemu katika nyumba ya Bwana, na katika nyumba ya mfalme, na ya wakuu, akampa mfalme wa Ashuru; asisaidiwe na jambo hilo.2 Chroniques 12.9 2 Rois 18.15-18.16 2 Rois 16.8-16.9 Proverbes 20.25
22 Na wakati alipofadhaishwa, akazidi kumwasi Bwana, huyo mfalme Ahazi.Esaïe 1.5 Esther 7.6 Psaumes 52.7 Ezéchiel 21.13 Psaumes 50.15
23 Kwani akaitolea dhabihu miungu ya Dameski iliyompiga, akasema, Kwa sababu miungu ya wafalme wa Shamu imewasaidia wao, mimi nitaitolea dhabihu, ili inisaidie mimi. Lakini ndiyo iliyomwangamiza yeye na Israeli wote.2 Chroniques 25.14 Jérémie 44.20-44.28 Habakuk 1.11 Esaïe 1.28 Jérémie 10.5
24 Tena Ahazi akakusanya vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, akavikata vipande vipande vyombo vya nyumba ya Mungu, akaifunga milango ya nyumba ya Bwana; akajifanyizia madhabahu katika kila pembe ya Yerusalemu.2 Chroniques 29.7 2 Chroniques 33.3-33.5 2 Rois 16.17-16.18 2 Chroniques 30.14 Actes 17.16
25 Na katika kila mji wa Yuda akafanya mahali pa juu pa kuifukizia miungu mingine uvumba, akamkasirisha Bwana, Mungu wa babaze.2 Chroniques 28.3
26 Basi mambo yake yote yaliyosalia, na njia zake zote, za kwanza na za mwisho, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.2 Rois 16.19-16.20 2 Chroniques 20.34 2 Chroniques 27.7-27.9
27 Ahazi akalala na babaze, wakamzika mjini, yaani, Yerusalemu; maana hawakumleta makaburini mwa wafalme wa Israeli; na Hezekia mwanawe akatawala mahali pake.2 Chroniques 21.20 2 Chroniques 24.25 1 Samuel 2.30 Proverbes 10.7 Esaïe 14.28

Cette Bible est dans le domaine public.