Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 25.31
Bible en Swahili de l’est


1 Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao;1 Chroniques 6.39 1 Chroniques 6.33 2 Rois 3.15 1 Samuel 10.5 Néhémie 12.27
2 wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme.1 Chroniques 25.6 1 Chroniques 25.1 Psaumes 81.1 Psaumes 83.1 Psaumes 78.1
3 Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu Bwana.1 Chroniques 16.41-16.42 1 Chroniques 9.16 Jérémie 33.11 Psaumes 92.1 1 Chroniques 25.21
4 Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;1 Chroniques 16.41-16.42 1 Chroniques 15.17 1 Chroniques 6.33 1 Chroniques 24.24 1 Chroniques 24.30
5 hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.1 Chroniques 21.9 Psaumes 127.3 1 Samuel 9.9 1 Chroniques 28.5 2 Samuel 24.11
6 Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa Bwana, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.1 Chroniques 25.1-25.3 Psaumes 68.25 1 Chroniques 15.19 Ephésiens 5.19 1 Chroniques 15.16
7 Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia Bwana, wote waliokuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.1 Chroniques 23.5
8 Wakatupiwa kura ya ulinzi wao, sawasawa wote, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.1 Chroniques 26.13 Néhémie 12.24 Actes 1.26 1 Chroniques 15.22 Lévitique 16.8
9 Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili; 10 ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 11 ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 12 ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 13 ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 14 ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 15 ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 16 ya kenda Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili; 17 ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 18 ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 19 ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 20 ya kumi na tatu Shebueli, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 21 ya kumi na nne Matithia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 22 ya kumi na tano Yeremothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 23 ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 24 ya kumi na saba Yoshbekasha, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 25 ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 26 ya kumi na kenda Malothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 27 ya ishirini Eliatha, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 28 ya ishirini na moja Hothiri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 29 ya ishirini na mbili Gidalti, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 30 ya ishirini na tatu Mahaziothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 31 ya ishirini na nne Romanti-ezeri, wanawe na nduguze, kumi na wawili.

Cette Bible est dans le domaine public.