1  Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda, akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa Wafilisti. 
2 Samuel 8.1-8.18  1 Samuel 27.4  2 Samuel 1.20  1 Samuel 5.8  
 2  Akapiga Moabu; na hao Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi wakaleta zawadi. 
Esaïe 11.14  Psaumes 60.8  2 Samuel 8.2  Juges 3.29-3.30  Psaumes 68.29-68.30  
 3  Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mamlaka yake kwenye mto wa Frati. 
2 Samuel 8.3  Psaumes 60.1  Exode 23.31  Genèse 15.18  2 Samuel 10.6  
 4  Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi saba elfu, na askari waendao kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia akawaweka. 
2 Samuel 8.4  1 Rois 10.26  Psaumes 20.7  Deutéronome 17.16  1 Rois 4.2  
 5  Na Washami wa Dameski walipokuja wamsaidie Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akapiga katika hao Washami watu ishirini na mbili elfu. 
1 Chroniques 19.6  1 Chroniques 18.3  Esaïe 8.9-8.10  1 Samuel 14.47  2 Samuel 8.5-8.6  
 6  Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda. 
Psaumes 18.43-18.44  Proverbes 21.31  1 Chroniques 18.2  1 Chroniques 17.8  Psaumes 121.8  
 7  Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumishi wa Hadadezeri akazileta Yerusalemu. 
1 Rois 14.26-14.28  2 Chroniques 12.9-12.10  2 Chroniques 9.15-9.16  1 Rois 10.16-10.17  
 8  Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyofanyizia Sulemani ile bahari ya shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba. 
2 Samuel 8.8  2 Chroniques 4.12-4.18  2 Chroniques 4.2-4.6  Jérémie 52.17-52.23  1 Chroniques 22.14  
 9  Hata aliposikia Tou, mfalme wa Hamathi, ya kuwa Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri, mfalme wa Soba, 
2 Samuel 8.9  
 10  akampeleka mwanawe Hadoramu kwa mfalme Daudi, ili kumsalimia, na kumbarikia, kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou; naye akaleta vyombo vya dhahabu, na fedha, na shaba, vya namna zote. 
2 Samuel 8.10  2 Chroniques 9.1  Esaïe 39.1  2 Chroniques 9.23-9.24  
 11  Hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa Bwana, pamoja na hiyo fedha na dhahabu, aliyoteka nyara kwa mataifa yote; kwa Edomu, na kwa Moabu, na kwa wana wa Amoni, na kwa Wafilisti, na kwa Amaleki. 
1 Chroniques 22.14  Psaumes 83.6-83.7  1 Chroniques 26.20  2 Rois 12.18  1 Samuel 27.8-27.9  
 12  Tena Abishai, mwana wa Seruya, akawapiga wa Waedomi katika Bonde la Chumvi watu kumi na nane elfu. 
1 Samuel 26.6  2 Samuel 20.6  2 Samuel 19.21-19.22  2 Chroniques 25.11  2 Samuel 3.30  
 13  Akaweka ngome katika Edomu; na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda, kila alikokwenda. 
1 Chroniques 18.6  Psaumes 121.7  1 Samuel 14.1  1 Samuel 10.5  2 Corinthiens 11.32  
 14  Basi Daudi akatawala juu ya Israeli wote; akawafanyia hukumu na haki watu wake wote. 
Jérémie 33.15  Esaïe 9.7  1 Chroniques 12.38  Esaïe 32.1-32.2  Psaumes 89.14  
 15  Na Yoabu mwana wa Seruya akawa juu ya jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe. 
1 Chroniques 11.6  2 Samuel 8.16  1 Rois 4.3  
 16  Na Sadoki mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki mwana wa Abiathari, walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi; 
2 Samuel 8.17  2 Samuel 20.25  1 Rois 4.3  1 Chroniques 24.6  1 Rois 2.35  
 17  na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; na wana wa Daudi walikuwa wakuu kumzunguka mfalme. 
2 Samuel 8.18  2 Samuel 15.18  2 Samuel 23.19-23.23  1 Rois 1.44  1 Chroniques 23.28