Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 18.17
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda, akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa Wafilisti.2 Samuel 8.1-8.18 1 Samuel 5.8 1 Samuel 27.4 2 Samuel 1.20
2 Akapiga Moabu; na hao Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi wakaleta zawadi.Psaumes 72.8-72.10 Esaïe 11.14 Psaumes 60.8 2 Samuel 8.2 Juges 3.29-3.30
3 Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mamlaka yake kwenye mto wa Frati.2 Samuel 8.3 Psaumes 60.1 1 Samuel 14.47 Exode 23.31 Genèse 15.18
4 Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi saba elfu, na askari waendao kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia akawaweka.2 Samuel 8.4 Josué 11.9 1 Rois 10.26 Psaumes 20.7 Deutéronome 17.16
5 Na Washami wa Dameski walipokuja wamsaidie Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akapiga katika hao Washami watu ishirini na mbili elfu.1 Chroniques 19.6 1 Rois 11.23-11.24 1 Chroniques 18.3 Esaïe 8.9-8.10 1 Samuel 14.47
6 Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.Psaumes 121.8 Psaumes 18.43-18.44 Proverbes 21.31 1 Chroniques 18.2 1 Chroniques 17.8
7 Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumishi wa Hadadezeri akazileta Yerusalemu.1 Rois 10.16-10.17 1 Rois 14.26-14.28 2 Chroniques 12.9-12.10 2 Chroniques 9.15-9.16
8 Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyofanyizia Sulemani ile bahari ya shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba.2 Samuel 8.8 2 Chroniques 4.12-4.18 2 Chroniques 4.2-4.6 Jérémie 52.17-52.23 1 Chroniques 22.14
9 Hata aliposikia Tou, mfalme wa Hamathi, ya kuwa Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri, mfalme wa Soba,2 Samuel 8.9
10 akampeleka mwanawe Hadoramu kwa mfalme Daudi, ili kumsalimia, na kumbarikia, kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou; naye akaleta vyombo vya dhahabu, na fedha, na shaba, vya namna zote.2 Samuel 8.10 2 Chroniques 9.23-9.24 2 Chroniques 9.1 Esaïe 39.1
11 Hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa Bwana, pamoja na hiyo fedha na dhahabu, aliyoteka nyara kwa mataifa yote; kwa Edomu, na kwa Moabu, na kwa wana wa Amoni, na kwa Wafilisti, na kwa Amaleki.2 Chroniques 5.1 1 Chroniques 22.14 Psaumes 83.6-83.7 1 Chroniques 26.20 2 Rois 12.18
12 Tena Abishai, mwana wa Seruya, akawapiga wa Waedomi katika Bonde la Chumvi watu kumi na nane elfu.1 Samuel 26.6 2 Samuel 10.10 2 Samuel 20.6 2 Samuel 19.21-19.22 2 Chroniques 25.11
13 Akaweka ngome katika Edomu; na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda, kila alikokwenda.1 Chroniques 18.6 2 Samuel 23.14 Psaumes 121.7 1 Samuel 14.1 1 Samuel 10.5
14 Basi Daudi akatawala juu ya Israeli wote; akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.2 Samuel 8.15 Jérémie 33.15 Esaïe 9.7 1 Chroniques 12.38 Esaïe 32.1-32.2
15 Na Yoabu mwana wa Seruya akawa juu ya jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe.1 Chroniques 11.6 2 Samuel 8.16 1 Rois 4.3
16 Na Sadoki mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki mwana wa Abiathari, walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;2 Samuel 8.17 2 Samuel 20.25 1 Rois 4.3 1 Chroniques 24.6 1 Rois 2.35
17 na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; na wana wa Daudi walikuwa wakuu kumzunguka mfalme.2 Samuel 8.18 2 Samuel 15.18 2 Samuel 20.7 2 Samuel 23.19-23.23 1 Rois 1.44

Cette Bible est dans le domaine public.