Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Apocalypse 7.10
Bible en Swahili de l’est


Le peuple de Dieu et le septième sceau

1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.
Matthieu 24.31 Daniel 7.2 Jérémie 49.36 Marc 13.27 Esaïe 27.8
2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,
2 Timothée 2.19 Apocalypse 7.3-7.8 Ephésiens 4.30 Ephésiens 1.13 Jean 6.27
3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
Apocalypse 14.1 Apocalypse 13.16 Ezéchiel 9.4 Apocalypse 9.4 Apocalypse 20.4
4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.
Apocalypse 14.3 Apocalypse 9.16 Apocalypse 14.1 Matthieu 19.28 Luc 22.30
5 Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
Nombres 1.4-1.15 Exode 1.2-1.4 Nombres 10.14-10.27 1 Corinthiens 2.1-2.2 Nombres 13.4-13.16
6 Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu.
Luc 2.36
7 Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.
Genèse 35.23 Nombres 26.14 Genèse 49.11 Nombres 1.22 Nombres 25.14
8 Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.
9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
Jean 12.13 Apocalypse 5.9 Lévitique 23.40 Apocalypse 7.13-7.15 Hébreux 12.22
10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.
Psaumes 3.8 Apocalypse 19.1 Apocalypse 12.10 Apocalypse 22.3 Apocalypse 21.5
11 Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,
Apocalypse 4.10 Apocalypse 4.6 Apocalypse 5.11-5.13 Apocalypse 4.4 Apocalypse 11.16
12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.
Apocalypse 5.12-5.14 Apocalypse 19.4 Psaumes 50.14 2 Corinthiens 9.11-9.12 Psaumes 116.17
13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?
Apocalypse 7.9 Apocalypse 4.10 Juges 13.6 Apocalypse 5.11 Jean 7.28
14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
1 Jean 1.7 Apocalypse 1.5 Hébreux 9.14 Hébreux 13.12 Zacharie 3.3-3.5
15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.
Apocalypse 22.3 Esaïe 4.5-4.6 Jean 1.14 Apocalypse 21.3-21.4 Exode 29.45
16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.
Esaïe 49.10 Esaïe 65.13 Psaumes 121.6 Matthieu 5.6 Marc 4.17
17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.
Apocalypse 21.4 Jean 4.14 Esaïe 25.8 Jean 10.11 Psaumes 23.1-23.2

Cette Bible est dans le domaine public.