Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Jean 4
Bible en Swahili de l’est


1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. 2 Pierre 2.1 1 Thessaloniciens 5.21 1 Jean 2.18 1 Timothée 4.1 Luc 12.57
2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. 1 Corinthiens 12.3 Jean 1.14 Jean 16.13-16.15 1 Jean 5.1 1 Timothée 3.16
3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. 1 Jean 2.22 1 Jean 2.18 2 Jean 1.7 2 Thessaloniciens 2.3-2.8
4 Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. 1 Jean 5.4 Jean 12.31 Romains 8.31 1 Jean 5.19 Romains 8.37
5 Hao ni wa dunia; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia Jean 17.14 Jean 8.23 Jean 17.16 Jean 3.31 2 Timothée 4.3
6 Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu. Jean 14.17 1 Corinthiens 14.37 Jean 10.27 Jean 18.37 1 Jean 4.1
7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 1 Jean 4.8 1 Jean 4.20-5.1 1 Jean 2.29 1 Thessaloniciens 4.9-4.10 1 Jean 2.10
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. 1 Jean 4.16 1 Jean 1.5 Psaumes 86.15 2 Corinthiens 13.11 1 Jean 4.7
9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. Jean 3.16 1 Jean 5.11 1 Jean 4.10 Jean 6.57 Romains 8.32
10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Ephésiens 2.4-2.5 1 Jean 2.2 1 Jean 3.1 Romains 5.8-5.10 1 Jean 4.19
11 Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. 1 Jean 3.23 Luc 10.37 Ephésiens 4.31-5.2 Matthieu 18.32-18.33 Colossiens 3.13
12 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. Jean 1.18 1 Jean 2.5 1 Jean 4.20 1 Timothée 6.16 Genèse 32.30
13 Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. 1 Jean 3.24 Jean 14.20-14.26 Galates 5.22-5.25 1 Jean 4.15-4.16 1 Corinthiens 3.16-3.17
14 Na sisi tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Jean 4.42 Jean 3.16-3.17 1 Jean 4.10 Jean 15.26-15.27 Jean 1.14
15 Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu. 1 Jean 5.5 Romains 10.9 1 Jean 3.24 1 Jean 4.2 1 Jean 4.12
16 Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. 1 Jean 3.1 1 Jean 4.8-4.10 Esaïe 64.4 1 Jean 3.24 1 Corinthiens 2.9
17 Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu. 1 Jean 4.12 1 Jean 2.5 1 Jean 2.28 1 Jean 3.19-3.21 Romains 8.29
18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo. 2 Timothée 1.7 Romains 8.15 1 Jean 4.12 Luc 1.74-1.75 Hébreux 12.28
19 Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. 1 Jean 4.10 Luc 7.47 Galates 5.22 Tite 3.3-3.5 Jean 3.16
20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. 1 Jean 3.17 1 Jean 4.12 1 Jean 2.4 1 Jean 2.9 1 Jean 2.11
21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. 1 Jean 3.11 Matthieu 22.37-22.39 1 Thessaloniciens 4.9 Lévitique 19.18 Jean 15.12

Cette Bible est dans le domaine public.