Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Pierre 4.3
Bible en Swahili de l’est


1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.1 Pierre 3.18 Romains 6.11 Galates 5.24 Ephésiens 6.13 Romains 6.2
2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.Ephésiens 4.22-4.24 Tite 3.3-3.8 Marc 3.35 2 Corinthiens 5.15 Romains 6.11
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;1 Thessaloniciens 4.5 Ephésiens 5.18 Ezéchiel 45.9 Actes 17.30 Galates 5.19
4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.1 Pierre 3.16 Jude 1.10 2 Pierre 2.22 1 Pierre 2.12 2 Pierre 2.12
5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.Actes 10.42 2 Timothée 4.1 Jacques 5.9 Romains 14.10-14.12 Ecclésiaste 12.14
6 Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.Tite 3.3-3.7 Ephésiens 2.3-2.5 Romains 8.9-8.11 Romains 8.2 1 Pierre 4.1-4.2
7 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.1 Pierre 1.13 1 Pierre 5.8 1 Thessaloniciens 5.6-5.8 Jacques 5.8-5.9 Tite 2.12
8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.Proverbes 10.12 Colossiens 3.14 Proverbes 17.9 1 Pierre 1.22 Jacques 5.20
9 Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika;Philippiens 2.14 Hébreux 13.2 Romains 12.13 1 Timothée 3.2 Tite 1.8
10 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.1 Corinthiens 4.1-4.2 1 Corinthiens 12.4-12.11 Luc 12.42 Romains 12.6-12.8 Tite 1.7
11 Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.1 Corinthiens 10.31 1 Pierre 5.11 1 Pierre 2.5 Romains 3.2 Actes 7.38
12 Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.1 Thessaloniciens 3.2-3.4 1 Pierre 1.6-1.7 2 Timothée 3.12 1 Pierre 5.9 Daniel 11.35
13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.Romains 8.17 Jacques 1.2-1.3 2 Corinthiens 4.10 Philippiens 3.10 2 Corinthiens 1.7
14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.1 Pierre 3.14 1 Pierre 3.16 Matthieu 5.11 Psaumes 146.5 Luc 6.22
15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.1 Thessaloniciens 4.11 2 Thessaloniciens 3.11 1 Timothée 5.13 1 Pierre 3.17 1 Pierre 2.19-2.20
16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.Actes 5.41 2 Timothée 1.12 Philippiens 1.29 1 Pierre 3.17-3.18 1 Pierre 4.19
17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?2 Thessaloniciens 1.8 Jérémie 25.29 Romains 2.9 1 Pierre 2.8 Ezéchiel 9.6
18 Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?Proverbes 11.31 Luc 23.31 2 Pierre 3.7 2 Pierre 2.5-2.6 Ezéchiel 18.24
19 Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.1 Pierre 3.17 Psaumes 31.5 Luc 23.46 2 Timothée 1.12 Psaumes 37.5

Cette Bible est dans le domaine public.