1  Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 
1 Pierre 3.18  Romains 6.11  Galates 5.24  Ephésiens 6.13  Romains 6.2  
 2  Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 
Ephésiens 4.22-4.24  Tite 3.3-3.8  Ephésiens 2.3  Marc 3.35  2 Corinthiens 5.15  
 3  Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; 
1 Thessaloniciens 4.5  Ephésiens 5.18  Ezéchiel 45.9  Actes 17.30  Galates 5.19  
 4  mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 
1 Pierre 3.16  Jude 1.10  2 Pierre 2.22  1 Pierre 2.12  2 Pierre 2.12  
 5  Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. 
Actes 10.42  2 Timothée 4.1  Jacques 5.9  Romains 14.10-14.12  Jude 1.14-1.15  
 6  Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai. 
Tite 3.3-3.7  Ephésiens 2.3-2.5  Romains 8.9-8.11  Romains 8.2  1 Pierre 4.1-4.2  
 7  Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. 
1 Pierre 1.13  1 Pierre 5.8  1 Thessaloniciens 5.6-5.8  Jacques 5.8-5.9  Tite 2.12  
 8  Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. 
Proverbes 10.12  Colossiens 3.14  Proverbes 17.9  1 Pierre 1.22  Jacques 5.20  
 9  Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika; 
Philippiens 2.14  Hébreux 13.2  Romains 12.13  1 Timothée 3.2  Tite 1.8  
 10  kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. 
1 Corinthiens 12.4-12.11  1 Corinthiens 4.1-4.2  Luc 12.42  Romains 12.6-12.8  Tite 1.7  
 11  Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina. 
1 Corinthiens 10.31  Actes 7.38  1 Pierre 5.11  1 Pierre 2.5  Romains 3.2  
 12  Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 
1 Thessaloniciens 3.2-3.4  1 Pierre 1.6-1.7  2 Timothée 3.12  1 Pierre 5.9  Daniel 11.35  
 13  Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 
Romains 8.17  Jacques 1.2-1.3  2 Corinthiens 4.10  Philippiens 3.10  2 Corinthiens 1.7  
 14  Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. 
1 Pierre 3.14  1 Pierre 3.16  Psaumes 146.5  Matthieu 5.11  Luc 6.22  
 15  Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. 
1 Thessaloniciens 4.11  2 Thessaloniciens 3.11  1 Timothée 5.13  1 Pierre 3.17  1 Pierre 2.19-2.20  
 16  Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo. 
Actes 5.41  2 Timothée 1.12  Philippiens 1.29  1 Pierre 3.17-3.18  1 Pierre 4.19  
 17  Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? 
2 Thessaloniciens 1.8  Jérémie 25.29  Romains 2.9  1 Pierre 2.8  Ezéchiel 9.6  
 18  Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi? 
Proverbes 11.31  Luc 23.31  2 Pierre 3.7  2 Pierre 2.5-2.6  Ezéchiel 18.24  
 19  Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu. 
1 Pierre 3.17  Psaumes 31.5  Luc 23.46  2 Timothée 1.12  Colossiens 1.16-1.20