Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Pierre 4
Bible en Swahili de l’est


1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. Romains 6.11 Galates 5.24 1 Pierre 3.18 Esaïe 1.16 Romains 13.12-13.14
2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. Tite 3.3-3.8 Ephésiens 4.22-4.24 2 Corinthiens 5.15 Romains 6.11 Romains 14.7
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; Ephésiens 5.18 1 Thessaloniciens 4.5 Actes 17.30 Galates 5.19 Esaïe 28.7
4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 1 Pierre 3.16 Jude 1.10 1 Pierre 2.12 2 Pierre 2.22 Actes 18.6
5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. Actes 10.42 2 Timothée 4.1 Jacques 5.9 Romains 14.10-14.12 Actes 17.31
6 Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai. Tite 3.3-3.7 Ephésiens 2.3-2.5 Romains 8.9-8.11 Romains 8.2 1 Pierre 4.1-4.2
7 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. 1 Pierre 1.13 1 Pierre 5.8 1 Thessaloniciens 5.6-5.8 Jacques 5.8-5.9 2 Timothée 4.5
8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. Proverbes 10.12 Colossiens 3.14 Proverbes 17.9 1 Pierre 1.22 Jacques 5.20
9 Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika; Philippiens 2.14 Hébreux 13.2 Romains 12.13 Tite 1.8 1 Timothée 3.2
10 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. 1 Corinthiens 12.4-12.11 1 Corinthiens 4.1-4.2 1 Corinthiens 4.7 Marc 10.45 Luc 19.13
11 Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina. 1 Corinthiens 10.31 Romains 3.2 Actes 7.38 1 Pierre 5.11 1 Pierre 2.5
12 Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 1 Thessaloniciens 3.2-3.4 2 Timothée 3.12 1 Pierre 1.6-1.7 1 Pierre 5.9 Daniel 11.35
13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. Romains 8.17 Jacques 1.2-1.3 2 Corinthiens 4.10 Philippiens 3.10 2 Corinthiens 1.7
14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. 1 Pierre 3.14 1 Pierre 3.16 Psaumes 146.5 Matthieu 5.11 Luc 6.22
15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. 1 Thessaloniciens 4.11 1 Timothée 5.13 2 Thessaloniciens 3.11 2 Timothée 2.9 Matthieu 5.11
16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo. Actes 5.41 Philippiens 1.29 2 Timothée 1.12 1 Pierre 3.17-3.18 1 Pierre 4.19
17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? 2 Thessaloniciens 1.8 Jérémie 25.29 Romains 2.9 1 Pierre 2.8 Ezéchiel 9.6
18 Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi? Proverbes 11.31 Luc 23.31 2 Pierre 2.5-2.6 Ezéchiel 18.24 2 Pierre 3.7
19 Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu. Luc 23.46 2 Timothée 1.12 1 Pierre 3.17 Psaumes 31.5 Psaumes 146.5-146.6

Cette Bible est dans le domaine public.