Conseils pour les temps difficiles
 1  Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 
1 Timothée 4.1-4.3  2 Pierre 3.3  2 Timothée 4.3  Ezéchiel 38.16  Michée 4.1  
 2  Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, 
Jude 1.16  Philippiens 2.21  Psaumes 10.3  2 Pierre 2.12  2 Timothée 3.4  
 3  wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, 
Romains 1.31  1 Timothée 3.11  Psaumes 22.6  Esaïe 60.14  Jude 1.18  
 4  wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; 
Philippiens 3.18-3.19  1 Timothée 3.6  Romains 16.18  1 Timothée 5.6  Romains 11.20  
 5  wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. 
Matthieu 23.27-23.28  Romains 2.20-2.24  Esaïe 29.13  Ezéchiel 33.30-33.32  1 Timothée 5.8  
 6  Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; 
Jude 1.4  Jude 1.18  Tite 1.11  Tite 3.3  Matthieu 23.13  
 7  wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli. 
2 Timothée 2.25  Esaïe 30.10-30.11  2 Timothée 4.3-4.4  Jean 5.44  Proverbes 14.6  
 8  Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani. 
Exode 7.11  1 Timothée 6.5  Actes 13.8-13.11  Tite 1.16  Actes 15.24  
 9  Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri. 
Exode 7.12  Exode 9.11  Jérémie 28.15-28.17  Actes 19.15-19.17  2 Timothée 3.8  
 10  Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu, 
1 Timothée 4.6  1 Timothée 6.11  Philippiens 2.22  Tite 2.7  Actes 2.42  
 11  na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote. 
Actes 13.45  Actes 14.5-14.6  Psaumes 34.19  2 Corinthiens 11.23-11.28  Actes 13.14  
 12  Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. 
Actes 14.22  1 Pierre 4.12-4.16  1 Pierre 2.20-2.21  1 Corinthiens 15.19  Tite 2.12  
 13  lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 
2 Pierre 2.20  Tite 3.3  Ezéchiel 14.9-14.10  2 Timothée 3.8  1 Timothée 4.1  
 14  Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; 
2 Timothée 1.13  1 Thessaloniciens 2.13  2 Timothée 2.2  1 Thessaloniciens 1.5  Hébreux 10.22  
 15  na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 
2 Timothée 1.5  2 Pierre 1.20-1.21  Psaumes 119.98-119.99  Proverbes 22.6  Psaumes 19.7  
 16  Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 
Romains 15.4  Hébreux 4.12  2 Pierre 1.19-1.21  Marc 12.24  Psaumes 19.7-19.11  
 17  ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. 
2 Timothée 2.21  1 Timothée 6.11  2 Corinthiens 9.8  Hébreux 10.24  Néhémie 2.18