Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Thessaloniciens 3
Bible en Swahili de l’est


1 Basi kwa hiyo, tulipokuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tuliona vema kuachwa Athene peke yetu. Actes 17.15 1 Thessaloniciens 3.5 1 Thessaloniciens 2.17 Jérémie 20.9 2 Corinthiens 2.13
2 Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu; Actes 14.22-14.23 Ephésiens 6.21-6.22 Philippiens 1.25 2 Corinthiens 8.23 2 Corinthiens 1.1
3 mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo. Actes 14.22 Actes 9.16 Actes 21.13 Matthieu 24.9-24.10 1 Corinthiens 15.58
4 Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mwajua. 1 Thessaloniciens 2.14 1 Thessaloniciens 2.2 Actes 20.24 2 Corinthiens 8.1-8.2 2 Thessaloniciens 1.4-1.6
5 Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida. Matthieu 4.3 Philippiens 2.16 Jacques 1.13-1.14 2 Corinthiens 2.11 Esaïe 49.4
6 Lakini Timotheo alipotujia hivi sasa kutoka kwenu, alituletea habari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote; mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi kuwaona ninyi. 1 Corinthiens 11.2 Proverbes 25.25 Actes 18.5 1 Thessaloniciens 1.3 Esaïe 52.7
7 Kwa sababu hiyo, ndugu, tulifarijiwa kwa habari zenu, katika msiba na dhiki yetu yote, kwa imani yenu. 2 Corinthiens 1.4 1 Corinthiens 4.9-4.13 Actes 17.4-17.10 1 Thessaloniciens 3.8-3.9 2 Timothée 3.10-3.12
8 Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana. 1 Corinthiens 16.13 Colossiens 1.23 Ephésiens 3.17 Actes 11.23 Galates 5.1
9 Maana ni shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu; 2 Corinthiens 9.15 Deutéronome 16.11 Psaumes 71.14-71.15 Deutéronome 12.18 2 Samuel 6.21
10 usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu, na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu? 2 Timothée 1.3 2 Corinthiens 13.9 Romains 1.10-1.12 2 Corinthiens 1.24 Apocalypse 4.8
11 Basi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu, atuongoze njia yetu tufike kwenu. 2 Thessaloniciens 2.16 Proverbes 3.5-3.6 1 Thessaloniciens 3.13 Romains 1.3 Matthieu 6.6
12 Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; Philippiens 1.9 2 Thessaloniciens 1.3 1 Thessaloniciens 4.9-4.10 1 Thessaloniciens 5.15 1 Jean 3.11-3.19
13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote. 1 Thessaloniciens 5.23 1 Thessaloniciens 2.19 Colossiens 1.22 Ephésiens 5.27 Zacharie 14.5

Cette Bible est dans le domaine public.