Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Deutéronome 25.15
Bible en Swahili de l’est


Les différends

1 Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu;
Proverbes 17.15 Deutéronome 17.8-17.9 Exode 23.6-23.7 Habakuk 1.13 Ezéchiel 44.24
2 na iwe, ikimpasa kupigwa yule mwovu, alazwe chini na mwamuzi, na kupigwa mbele ya uso wake, kwa kadiri ya uovu wake, kwa kuhesabu.
Luc 12.47-12.48 1 Pierre 2.24 1 Pierre 2.20 Actes 16.22-16.24 Matthieu 10.17
3 Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi.
Job 18.3 Luc 18.9-18.12 Jacques 2.2-2.3 2 Corinthiens 11.24-11.25 Luc 15.30
4 Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.
Proverbes 12.10 1 Corinthiens 9.9-9.10 Osée 10.11 1 Timothée 5.17-5.18 Esaïe 28.27

La descendance d’un frère mort

5 Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe.
Marc 12.19 Luc 20.28 Matthieu 22.24 Genèse 38.8-38.9 Ruth 1.12-1.13
6 Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli.
Deutéronome 29.20 Genèse 28.8-28.10 Ruth 4.10-4.12 Psaumes 9.5 Psaumes 109.13
7 Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu.
Ruth 4.5-4.6 Ruth 4.1-4.2
8 Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu,
Ruth 4.6
9 ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi.
Ruth 4.7-4.8 Nombres 12.14 Esaïe 50.6 Job 30.10 Matthieu 27.30
10 Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu.
11 Washindanapo waume wao kwa wao, akakaribia mke wa mmojawapo, ili kumwokoa mumewe katika mkono wa ampigaye, yule mke akatoa mkono wake, na kumkamata tupu yake;
1 Timothée 2.9 Romains 3.8
12 umkate ule mkono wake, lisiwe na huruma jicho lako.
Deutéronome 19.13 Deutéronome 19.21 Deutéronome 7.2

Une mesure juste

13 Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako.
Proverbes 11.1 Amos 8.5 Lévitique 19.35-19.37 Proverbes 16.11 Proverbes 20.10
14 Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako.
15 Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.
Exode 20.12 Deutéronome 4.40 Deutéronome 6.18 Psaumes 34.12 Deutéronome 11.9
16 Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.
Proverbes 11.1 Deutéronome 22.5 Deutéronome 18.12 1 Thessaloniciens 4.6 1 Corinthiens 6.9-6.11

Jugement futur d’Amalek

17 Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri;
Exode 17.8-17.16 Nombres 25.17-25.18 Nombres 24.20
18 jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu.
Romains 3.18 Psaumes 36.1 Proverbes 16.6 Néhémie 5.15 Néhémie 5.9
19 Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.
Exode 17.14 Deutéronome 9.14 Josué 23.1 1 Samuel 27.8 1 Samuel 30.1-30.7

Cette Bible est dans le domaine public.