Rôle de Paul
 1  Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; 
Colossiens 1.24  Ephésiens 4.1  Philémon 1.9  2 Timothée 1.8  Ephésiens 6.20  
 2  ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; 
2 Timothée 1.11  Ephésiens 4.7  Romains 1.5  Ephésiens 1.10  Galates 1.15-1.16  
 3  ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. 
Ephésiens 3.9  Romains 16.25  Galates 1.12  Actes 22.17  Ephésiens 1.9-1.11  
 4  Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. 
2 Corinthiens 11.6  Colossiens 4.3  1 Corinthiens 4.1  Ephésiens 6.19  1 Corinthiens 2.6-2.7  
 5  Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; 
Jude 1.17  2 Pierre 3.2  Tite 1.1-1.3  Actes 10.28  Ephésiens 2.20  
 6  ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; 
Romains 8.15-8.17  Galates 3.14  Colossiens 2.19  Ephésiens 5.30  Ephésiens 5.7  
 7  Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. 
Ephésiens 1.19  Ephésiens 3.20  Ephésiens 3.2  1 Timothée 1.14-1.15  2 Corinthiens 3.6  
 8  Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; 
1 Corinthiens 15.9  1 Timothée 1.13  1 Timothée 2.7  2 Timothée 1.11  Philippiens 2.3  
 9  na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; 
Colossiens 1.26  Matthieu 13.35  2 Timothée 1.9  Romains 16.25-16.26  Colossiens 3.3  
 10  ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; 
1 Pierre 1.12  Ephésiens 1.21  1 Corinthiens 2.7  Ephésiens 1.3  Romains 11.33  
 11  kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu. 
Ephésiens 1.11  2 Timothée 1.9  Esaïe 14.24-14.27  Romains 9.11  Ephésiens 1.9  
 12  Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini. 
Hébreux 4.14-4.16  Ephésiens 2.18  Romains 5.2  Hébreux 10.19-10.22  Jean 14.6  
 13  Basi naomba msikate tamaa kwa sababu ya dhiki zangu kwa ajili yenu, zilizo utukufu kwenu. 
Colossiens 1.24  Ephésiens 3.1  Esaïe 40.30-40.31  Philippiens 1.12-1.14  2 Corinthiens 1.6  
Prière de Paul pour les Éphésiens
 14  Kwa hiyo nampigia Baba magoti, 
Ephésiens 1.16-1.19  Actes 21.5  Esdras 9.5  Luc 22.41  Psaumes 95.6  
 15  ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, 
Ephésiens 1.21  Ephésiens 1.10  Actes 11.26  Apocalypse 5.8-5.14  Jérémie 33.16  
 16  awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. 
Colossiens 1.11  Philippiens 4.13  Esaïe 40.29-40.31  Philippiens 4.19  Esaïe 41.10  
 17  Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; 
Jean 14.23  Colossiens 2.7  Colossiens 1.23  Galates 2.20  1 Jean 4.16  
 18  ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; 
Psaumes 103.11-103.12  Ephésiens 1.15  Galates 2.20  Job 11.7-11.9  Jean 15.13  
 19  na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. 
Ephésiens 1.23  Colossiens 1.10  Colossiens 2.9-2.10  Apocalypse 22.3-22.5  Galates 2.20  
 20  Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; 
2 Corinthiens 9.8  Romains 4.21  Jude 1.24  1 Corinthiens 2.9  Ephésiens 1.19  
 21  naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina. 
Romains 11.36  Jude 1.25  1 Pierre 5.11  Philippiens 4.20  Romains 16.27