Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nombres 28.2
Bible en Swahili de l’est


Rappel des engagements envers l’Éternel

L’holocauste perpétuel

1 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
2 Waagize hao wana wa Israeli, uwaambie, Matoleo yangu, chakula changu cha sadaka zangu zisongezwazo kwa moto, za harufu ya kupendeza kwangu mimi, mtaangalia kuzisongeza kwangu wakati wake upasao.
Lévitique 3.11 Genèse 8.21 Ephésiens 5.2 Lévitique 1.9 Exode 29.18
3 Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsongezea Bwana; wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu, wawili kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote.
Lévitique 6.9 Ezéchiel 46.13-46.15 Apocalypse 13.8 Jean 1.29 Daniel 11.31
4 Mwana-kondoo mmoja utamsongeza asubuhi, na mwana-kondoo wa pili utamsongeza jioni;
Psaumes 141.2 Esdras 9.4-9.5 1 Rois 18.29 Exode 12.6 Daniel 9.21
5 pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa.
Lévitique 2.1 Exode 16.36 Exode 29.38-29.42 Nombres 15.4-15.5
6 Ni sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, iliyoamriwa huko katika mlima wa Sinai iwe harufu ya kupendeza, sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa moto.
Amos 5.25 2 Chroniques 31.3 Esdras 3.4 Psaumes 50.8 Lévitique 6.9
7 Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia Bwana katika mahali hapo patakatifu.
Exode 29.42 Philippiens 2.17 Nombres 15.7 Nombres 28.14 Nombres 15.5
8 Na mwana-kondoo wa pili utamsongeza wakati wa jioni; kama ile sadaka ya unga iliyosongezwa asubuhi, na kama sadaka yake ya kinywaji, ndivyo utakavyoisongeza, ni sadaka ya kusongezwa kwa moto, ni harufu ya kupendeza kwa Bwana.

Les sacrifices du sabbat

9 Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo wawili, waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, pamoja na sehemu ya kumi mbili za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji;
Esaïe 58.13 Exode 20.8-20.11 Apocalypse 1.10 Ezéchiel 20.12 Psaumes 92.1-92.4
10 hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Ezéchiel 46.4-46.5 Nombres 29.19 Nombres 29.11 Nombres 28.23 Nombres 28.3

Les sacrifices mensuels

11 Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba;
Nombres 10.10 Ezéchiel 46.6 Esaïe 1.13-1.14 Colossiens 2.16 2 Chroniques 2.4
12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja;
Nombres 15.4-15.12 Nombres 29.10 Ezéchiel 46.5-46.7
13 na sehemu ya kumi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwana-kondoo; kuwa sadaka ya kuteketezwa ya harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.
14 Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng’ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo mume, na robo ya hini kwa mwana-kondoo; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka.
15 Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa Bwana itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Nombres 28.3 Nombres 28.22 Nombres 15.24 Lévitique 4.23 Lévitique 16.15

Les sacrifices de la Pâque

16 Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni pasaka ya Bwana.
Exode 12.18 Exode 12.2-12.11 Deutéronome 16.1-16.8 Lévitique 23.5-23.8 Matthieu 26.2
17 Siku ya kumi na tano ya mwezi huo patakuwa na sikukuu; mkate usiotiwa chachu utaliwa muda wa siku saba.
Lévitique 23.6 Exode 34.18 Exode 12.15-12.17 Deutéronome 16.3-16.8 Exode 23.15
18 Siku ya kwanza patakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi;
Exode 12.16 Lévitique 23.7-23.8
19 lakini mtaisongeza sadaka kwa njia ya moto, sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana; ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu;
Deutéronome 15.21 Nombres 29.8 Nombres 28.31 Lévitique 22.20 Ezéchiel 45.21-45.25
20 pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta; mtasongeza sehemu ya kumi tatu kwa ng’ombe mmoja, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume;
21 na sehemu ya kumi moja utasongeza kwa kila mwana-kondoo, wale wana-kondoo saba;
22 tena mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
Romains 8.3
23 Mtasongeza wanyama hao zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, iliyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote.
Nombres 28.3 Nombres 28.10
24 Mtasongeza sadaka kwa mfano huu kila siku muda wa siku saba, chakula cha sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana; itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
25 Na siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi.
Lévitique 23.8 Exode 13.6 Exode 12.16 Nombres 28.18 Lévitique 23.35-23.36

Les sacrifices de la fête des moissons

26 Tena katika siku ya malimbuko, hapo mtakapomsongezea Bwana sadaka ya unga mpya katika sikukuu yenu ya majuma mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi;
Exode 23.16 Exode 34.22 Lévitique 23.10 Lévitique 23.15-23.21 Deutéronome 16.9-16.11
27 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe waume wadogo wawili, kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba;
Lévitique 23.18-23.19 Nombres 28.11 Nombres 28.19
28 pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng’ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume,
29 na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo, wa wale wana-kondoo saba;
30 na mbuzi mume mmoja, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
Nombres 28.22 Nombres 28.15 1 Pierre 3.18 Nombres 15.24 Galates 3.13
31 Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji.
Nombres 28.19 Nombres 28.3 Malachie 1.13-1.14

Cette Bible est dans le domaine public.