Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nahum 1.11
Bible en Swahili de l’est


1 Ufunuo juu ya Ninawi. Kitabu cha maono aliyoyaona Nahumuu, Mwelkoshi.Sophonie 2.13 Zacharie 9.1 Jonas 1.2 Esaïe 13.1 Genèse 10.11
2 Bwana ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; Bwana hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.Exode 20.5 Zacharie 8.2 Psaumes 94.1 Josué 24.19 Deutéronome 4.24
3 Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.Psaumes 147.5 Psaumes 104.3 Néhémie 9.17 Jacques 1.19 Exode 34.6-34.7
4 Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote; Bashani hulegea, na Karmeli; hulegea nalo ua la Lebanoni.Esaïe 33.9 Psaumes 106.9 Matthieu 8.26 Ezéchiel 30.12 Esaïe 44.27
5 Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.Michée 1.4 2 Samuel 22.8 Jérémie 4.24 Esaïe 64.1-64.2 Habakuk 3.10
6 Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.Malachie 3.2 Jérémie 10.10 Nahum 1.2 Ezéchiel 30.16 Apocalypse 6.17
7 Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.2 Timothée 2.19 Jérémie 33.11 Jean 10.27 Psaumes 1.6 Jean 10.14
8 Lakini kwa gharika ifurikayo atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatia adui zake hata gizani.Esaïe 8.22 Amos 8.8 Esaïe 28.17 Sophonie 2.13 Esaïe 8.7-8.8
9 Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.Psaumes 33.10 Psaumes 21.11 Psaumes 2.1-2.4 2 Corinthiens 10.5 Proverbes 21.30
10 Kwa maana wangawa kama miiba iliyotatana, na kunyweshwa kana kwamba ni katika kunywa kwao, wataliwa kabisa kama mabua makavu.Michée 7.4 Malachie 4.1 Nahum 3.11 2 Samuel 23.6-23.7 Esaïe 5.24
11 Ametoka mmoja kwako, aniaye mabaya juu ya Bwana, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.Nahum 1.9 Esaïe 10.7-10.15 2 Chroniques 32.15-32.19 2 Rois 18.30 2 Chroniques 13.7
12 Bwana asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.Esaïe 30.19 Lamentations 3.31-3.32 Esaïe 8.8 Exode 12.12 2 Rois 19.37
13 Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitakupasulia mafungo yako.Esaïe 9.4 Esaïe 10.27 Psaumes 107.14 Jérémie 5.5 Jérémie 2.20
14 Tena Bwana ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.Psaumes 109.13 2 Rois 19.37 Ezéchiel 32.22-32.23 Esaïe 46.1-46.2 Jérémie 50.2
15 Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.Romains 10.15 Esaïe 52.7 Esaïe 29.7-29.8 Esaïe 40.9-40.10 Nahum 1.11-1.12

Cette Bible est dans le domaine public.