Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Lamentations 4.2
Bible en Swahili de l’est


1 Jinsi dhahabu ilivyoacha kung’aa, Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika! Mawe ya patakatifu yametupwa Mwanzo wa kila njia.Ezéchiel 7.19-7.22 Esaïe 1.21 Lamentations 2.19 2 Rois 25.9-25.10 Esaïe 14.12
2 Wana wa Sayuni wenye thamani, Walinganao na dhahabu safi, Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo, Kazi ya mikono ya mfinyanzi!Jérémie 19.11 Esaïe 30.14 Zacharie 9.13 Lamentations 5.12 Romains 9.21-9.23
3 Hata mbwa-mwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani.Ezéchiel 5.10 Esaïe 49.15 Lamentations 4.10 Luc 23.28-23.29 Lévitique 26.29
4 Ulimi wa mtoto anyonyaye Wagandamana na kaakaa lake kwa kiu; Watoto wachanga waomba chakula, Wala hakuna hata mmoja awamegeaye.Psaumes 22.15 Lamentations 2.11-2.12 Psaumes 137.6 Deutéronome 32.24 Lamentations 1.11
5 Wale waliokula vitu vya anasa Wameachwa peke yao njiani; Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu Wakumbatia jaa.Amos 6.3-6.7 Luc 7.25 2 Samuel 1.24 Luc 15.16 Luc 16.19
6 Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwa Kuliko dhambi ya Sodoma, Uliopinduliwa kama katika dakika moja, Wala mikono haikuwekwa juu yake.Genèse 19.25 Luc 10.12 Lamentations 4.9 Matthieu 11.23-11.24 Daniel 9.12
7 Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi.Psaumes 51.7 Cantique 5.10 Juges 16.17 Amos 2.11-2.12 Juges 13.5
8 Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa; Hawajulikani katika njia kuu; Ngozi yao yagandamana na mifupa yao Imekauka, imekuwa kama mti.Lamentations 5.10 Psaumes 102.3-102.5 Job 30.30 Job 19.20 Psaumes 119.83
9 Heri wale waliouawa kwa upanga Kuliko wao waliouawa kwa njaa; Maana hao husinyaa, wakichomwa Kwa kukosa matunda ya mashamba.Lévitique 26.39 Ezéchiel 24.23 Jérémie 16.4 Ezéchiel 33.10
10 Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.Lamentations 2.20 Esaïe 49.15 Jérémie 19.9 Ezéchiel 5.10 Lamentations 4.3
11 Bwana ameitimiza kani yake, Ameimimina hasira yake kali; Naye amewasha moto katika Sayuni Ulioiteketeza misingi yake.Jérémie 7.20 Ezéchiel 22.31 Lamentations 2.17 Jérémie 17.27 Jérémie 9.9-9.11
12 Wafalme wa dunia hawakusadiki, Wala wote wakaao duniani, Ya kwamba mtesi na adui wangeingia Katika malango ya Yerusalemu.Deutéronome 29.24-29.28 1 Rois 9.8-9.9 Psaumes 48.4-48.6 Jérémie 21.13
13 Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wake Na maovu ya makuhani wake, Walioimwaga damu ya wenye haki Katikati yake.Jérémie 5.31 Jérémie 6.13 Jérémie 26.8-26.9 Lamentations 2.14 Ezéchiel 22.26-22.28
14 Hutanga-tanga njiani kama vipofu, Wametiwa unajisi kwa damu; Hata ikawa watu wasiweze Kuyagusa mavazi yao.Jérémie 2.34 Deutéronome 28.28-28.29 Esaïe 56.10 Esaïe 1.15 Nombres 19.16
15 Watu waliwapigia kelele, Ondokeni, Uchafu, Ondokeni, ondokeni, msiguse; Walipokimbia na kutanga-tanga, watu walisema kati ya mataifa, Hawatakaa hapa tena.Lévitique 13.45-13.46
16 Hasira ya Bwana imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao.Lamentations 5.12 Esaïe 9.14-9.16 2 Chroniques 36.17 Deutéronome 32.26 Psaumes 106.44
17 Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa.Ezéchiel 29.16 Ezéchiel 29.6-29.7 Esaïe 20.5 2 Rois 24.7 Jérémie 8.20
18 Wanatuvizia hatua zetu, Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu; Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia; Maana mwisho wetu umefika.Amos 8.2 Ezéchiel 7.2-7.12 Jérémie 16.16 Lamentations 3.52 Ezéchiel 12.22-12.23
19 Waliotufuatia ni wepesi Kuliko tai za mbinguni; Hao walitufuatia milimani, Nao walituotea jangwani.Esaïe 5.26-5.28 Habakuk 1.8 Jérémie 4.13 Esaïe 30.16-30.17 Deutéronome 28.49
20 Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao;Ambaye kwa habari zake tulisema,Chini ya kivuli chake tukakaa kati ya mataifa.2 Samuel 19.21 Jérémie 39.5 Genèse 2.7 Ezéchiel 12.13 2 Samuel 1.14
21 Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi.Job 1.1 Amos 1.11 Psaumes 137.7 Ezéchiel 25.6 Ezéchiel 35.11-35.15
22 Uovu wako umetimia, Ee binti Sayuni; Hatakuhamisha tena; Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu; Atazivumbua dhambi zako.Esaïe 40.2 Psaumes 137.7 Jérémie 32.40 Lamentations 4.6 Esaïe 60.18

Cette Bible est dans le domaine public.