Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 33.9
Bible en Swahili de l’est


1 Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.Esaïe 21.2 Matthieu 7.2 Jérémie 25.12-25.14 Esaïe 24.16 Esaïe 10.12
2 Ee Bwana, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu kila asubuhi,na wokovu wetu pia wakati wa taabu.Esaïe 25.9 Esaïe 30.18-30.19 Esaïe 26.8 Psaumes 27.13-27.14 Psaumes 50.15
3 Kabila za watu wamekimbia wakisikia kelele za fujo; mataifa wametawanyika ulipojiinua nafsi yako.Esaïe 17.12-17.14 Esaïe 59.16-59.18 Esaïe 10.32-10.34 Esaïe 37.11-37.18 Psaumes 46.6
4 Na mateka yako yatakumbwa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige.Joël 2.9 Esaïe 33.23 2 Chroniques 20.25 Joël 2.25 2 Chroniques 14.13
5 Bwana ametukuka; kwa maana anakaa juu; amejaza Sayuni hukumu na haki.Esaïe 2.17 Esaïe 33.10 Exode 15.1 Exode 18.11 2 Chroniques 31.20-31.21
6 Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha Bwana ni hazina yake ya akiba.Matthieu 6.33 Psaumes 112.1-112.3 Proverbes 24.3-24.7 Esaïe 51.6 Proverbes 19.23
7 Angalia, mashujaa wao wanalia nje, wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu.Esaïe 36.22 2 Rois 18.18 Esaïe 36.3 2 Rois 18.37-19.3
8 Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.Juges 5.6 Esaïe 10.29-10.31 1 Samuel 17.10 Luc 18.2-18.4 Esaïe 36.1
9 Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani.Esaïe 35.2 Esaïe 65.10 Nahum 1.4 Esaïe 3.26 Jérémie 50.19
10 Basi, sasa nitasimama; asema Bwana; sasa nitajiinua, sasa nitajitukuza.Psaumes 12.5 Esaïe 10.33 Esaïe 10.16 Esaïe 42.13-42.14 Esaïe 2.21
11 Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto utakaowateketeza wenyewe.Esaïe 59.4 Psaumes 7.14 Jacques 1.15 Job 15.35 Esaïe 17.13
12 Nao mataifa watakuwa kama kuchoma chokaa, kama miiba iliyokatika, iteketezwayo motoni.Esaïe 27.4 2 Samuel 23.6-23.7 Esaïe 9.18 Amos 2.1 Esaïe 10.17
13 Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uweza wangu.Psaumes 48.10 Esaïe 49.1 Ephésiens 2.11-2.18 Esaïe 18.3 Daniel 3.27-4.3
14 Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?Hébreux 12.29 Matthieu 25.41 Apocalypse 14.10 Matthieu 25.46 Esaïe 66.24
15 Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.Psaumes 119.37 2 Pierre 2.14-2.16 Psaumes 26.1-26.2 Psaumes 24.4-24.5 Job 31.29-31.31
16 Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.Esaïe 32.18 Luc 12.29-12.31 Habakuk 3.19 Proverbes 1.33 Psaumes 91.1-91.10
17 Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana.Esaïe 6.5 Jean 14.21 Jean 1.14 1 Jean 3.2 Hébreux 11.13-11.15
18 Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara?2 Rois 18.14 1 Corinthiens 1.20 2 Rois 18.31 1 Samuel 25.33-25.36 2 Rois 15.19
19 Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuelewa nayo.Esaïe 28.11 Deutéronome 28.49-28.50 Jérémie 5.15 2 Rois 19.32 Ezéchiel 3.5-3.6
20 Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang’olewa, wala kamba zake hazitakatika.Psaumes 46.5 Esaïe 32.18 Esaïe 54.2 Matthieu 16.18 Psaumes 125.1-125.2
21 Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo.Psaumes 46.4-46.5 2 Corinthiens 4.4-4.6 Esaïe 66.12 Psaumes 29.3 Actes 7.2
22 Kwa maana Bwana ndiye mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.Jacques 4.12 Psaumes 89.18 Esaïe 25.9 Zacharie 9.9 Esaïe 12.2
23 Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka.2 Rois 7.8 Psaumes 68.12 1 Corinthiens 1.27 Actes 27.40-27.41 1 Samuel 30.10
24 Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.Jérémie 50.20 Michée 7.18-7.19 1 Jean 1.7-1.9 Esaïe 44.22 Esaïe 58.8

Cette Bible est dans le domaine public.