Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 94.11
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, Mungu wa kisasi, Mungu wa kisasi, uangaze,Nahum 1.2 Deutéronome 32.35 Esaïe 35.4 Romains 12.19 Psaumes 80.1
2 Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze, Uwape wenye kiburi stahili zao.Psaumes 31.23 Genèse 18.25 Psaumes 7.6 Esaïe 37.36-37.38 Daniel 4.37
3 Bwana, hata lini wasio haki, Hata lini wasio haki watashangilia?Job 20.5 Apocalypse 6.10 Psaumes 79.5 Psaumes 43.2 Esther 7.10
4 Je! Wote watendao uovu watatoa maneno, Na kusema majivuno, na kufanya kiburi?Psaumes 31.18 Psaumes 52.1 Esaïe 10.13-10.15 Psaumes 59.7 Matthieu 12.34
5 Ee Bwana, wanawaseta watu wako; Wanautesa urithi wako;Esaïe 3.15 Jérémie 51.34 Apocalypse 17.6 Jérémie 50.11 Esaïe 52.5
6 Wanamwua mjane na mgeni; Wanawafisha yatima.Esaïe 10.2 Esaïe 13.15-13.18 Jérémie 7.6 Ezéchiel 22.7 Jérémie 22.3
7 Nao husema, Bwana haoni; Mungu wa Yakobo hafikiri.Psaumes 10.11-10.13 Job 22.12-22.13 Psaumes 59.7 Ezéchiel 9.9 Luc 18.3-18.4
8 Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini; Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?Psaumes 92.6 Psaumes 49.10 Proverbes 8.5 Jérémie 8.6-8.8 Romains 3.11
9 Aliyelitia sikio mahali pake asisikie? Aliyelifanya jicho asione?Exode 4.11 Proverbes 20.12 Psaumes 17.3 Psaumes 44.21 Psaumes 11.4
10 Awaadibuye mataifa asikemee? Amfundishaye mwanadamu asijue?Job 35.11 Esaïe 28.26 Psaumes 44.2 Psaumes 10.16 Esaïe 37.36
11 Bwana anajua mawazo ya mwanadamu, Ya kuwa ni ubatili.1 Corinthiens 3.20 Romains 1.21-1.22 1 Corinthiens 1.21 Psaumes 49.10-49.13 Job 11.11-11.12
12 Ee Bwana, heri mtu yule umwadibuye, Na kumfundisha kwa sheria yako;Proverbes 3.11-3.12 Job 5.17 Hébreux 12.5-12.11 Psaumes 119.71 1 Corinthiens 11.32
13 Upate kumstarehesha siku za mabaya, Hata asiye haki atakapochimbiwa shimo.Psaumes 55.23 Psaumes 9.15 Apocalypse 14.13 2 Pierre 2.9 Habakuk 3.16
14 Kwa kuwa Bwana hatawatupa watu wake, Wala hutauacha urithi wake,1 Samuel 12.22 Psaumes 37.28 Romains 11.1-11.2 Deutéronome 32.9 Hébreux 13.5
15 Maana hukumu itairejea haki, Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.Michée 7.9 Psaumes 7.8-7.9 Job 23.11-23.12 Esaïe 42.3 Psaumes 37.34
16 Ni nani atakayesimama Kwa ajili yangu juu ya wabaya? Ni nani atakayenisaidia Juu yao wafanyao maovu?2 Rois 10.15 1 Rois 18.39-18.40 Jérémie 5.1 Jean 7.50-7.51 Psaumes 17.13
17 Kama Bwana asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.Psaumes 124.1-124.2 Psaumes 31.17 Psaumes 118.13 Psaumes 13.3 Psaumes 142.4-142.5
18 Niliposema, Mguu wangu unateleza; Ee Bwana, fadhili zako zilinitegemeza.Psaumes 38.16 Psaumes 37.23-37.24 Psaumes 121.3 Esaïe 41.10 Psaumes 119.116-119.117
19 Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu, Faraja zako zaifurahisha roho yangu.Psaumes 77.2-77.10 Psaumes 61.2 Habakuk 3.16-3.18 Psaumes 63.5-63.6 1 Pierre 1.7-1.8
20 Je! Kiti cha udhalimu kishirikiane nawe, Kitungacho madhara kwa njia ya sheria?Psaumes 58.2 Amos 6.3 Esaïe 10.1 Esaïe 1.11-1.20 1 Rois 12.32
21 Huishambulia nafsi yake mwenye haki, Na kuihukumu damu isiyo na hatia.Proverbes 17.15 Matthieu 27.1 Exode 23.7 Psaumes 59.3 Actes 7.58-7.60
22 Lakini Bwana amekuwa ngome kwangu, Na Mungu wangu mwamba wangu wa kukimbilia.Psaumes 18.2 Psaumes 59.9 Psaumes 62.2 Psaumes 9.9 Psaumes 59.16-59.17
23 Naye atawarudishia uovu wao, Atawaangamiza katika ubaya wao, Naam, Bwana, Mungu wetu, atawaangamiza.Psaumes 7.16 Proverbes 2.22 Proverbes 14.32 Psaumes 9.16-9.17 1 Samuel 26.10-26.11

Cette Bible est dans le domaine public.