Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 86.5
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, utege sikio lako unijibu, Maana mimi ni maskini na mhitajiPsaumes 40.17 Psaumes 31.2 Psaumes 34.6 Psaumes 10.14 Psaumes 140.12
2 Unihifadhi nafsi yangu, Maana mimi ni mcha Mungu. Wewe uliye Mungu wangu, Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini.Psaumes 4.3 Ephésiens 1.12-1.13 Psaumes 31.1 Jean 10.27-10.29 Romains 9.18
3 Wewe, Bwana, unifadhili, Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.Psaumes 57.1 Psaumes 88.9 Psaumes 25.5 Psaumes 56.1 Psaumes 4.1
4 Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.Psaumes 25.1 Psaumes 143.8 Esaïe 61.3 Esaïe 65.18 Psaumes 62.8
5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.Joël 2.13 Psaumes 103.8 Exode 34.6 Néhémie 9.17 Psaumes 130.7
6 Ee Bwana, uyasikie maombi yangu; Uisikilize sauti ya dua zangu.Psaumes 5.1-5.2 Psaumes 130.2 Psaumes 55.1 Psaumes 17.1
7 Siku ya mateso yangu nitakuita, Kwa maana utaniitikia.Psaumes 50.15 Jonas 2.2 Psaumes 17.6 Psaumes 34.4-34.6 Hébreux 5.7
8 Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana, Wala matendo mfano wa matendo yako.Exode 15.11 Psaumes 89.6 Deutéronome 3.24 Deutéronome 4.34 Esaïe 40.18
9 Mataifa yote uliowafanya watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana, Watalitukuza jina lako;Psaumes 66.4 Apocalypse 15.4 Esaïe 66.23 Esaïe 2.2-2.4 Psaumes 102.15
10 Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, Ndiwe Mungu peke yako.Psaumes 72.18 Marc 12.29 Esaïe 37.16 1 Corinthiens 8.4 Deutéronome 32.39
11 Ee Bwana, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;Jérémie 32.38-32.39 Psaumes 5.8 Job 34.32 Psaumes 26.3 1 Corinthiens 6.17
12 Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele.Deutéronome 6.5 Romains 15.6 1 Corinthiens 10.31 1 Corinthiens 6.20 Psaumes 104.33
13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.Psaumes 103.8-103.12 Luc 1.58 1 Thessaloniciens 1.10 Psaumes 88.6 Psaumes 30.3
14 Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia; Mkutano wa wakatili wamenitafuta roho. Wala hawakukuweka Wewe Mbele ya macho yao.Psaumes 54.3 Psaumes 10.4 2 Samuel 16.20-17.1 2 Samuel 17.14 2 Samuel 15.1-15.12
15 Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.Néhémie 9.17 Psaumes 111.4 Psaumes 86.5 Psaumes 103.8 Nombres 14.18
16 Unielekee na kunifadhili mimi; Mpe mtumishi wako nguvu zako, Umwokoe mwana wa mjakazi wako.Psaumes 25.16 Psaumes 116.16 Esaïe 40.29-40.31 Psaumes 84.5 Luc 1.38
17 Unifanyie ishara ya wema, Wanichukiao waione na kuaibishwa. Kwa kuwa Wewe, Bwana, Umenisaidia na kunifariji.Psaumes 41.10-41.11 Psaumes 40.1 Psaumes 71.20-71.21 Juges 6.17 1 Corinthiens 5.5

Cette Bible est dans le domaine public.