Invitation à écouter le Seigneur
 1  Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. 
Psaumes 66.1  Jérémie 31.7  Psaumes 8.1  Psaumes 46.11  Philippiens 4.13  
 2  Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda. 
Psaumes 92.3  Exode 15.20  Psaumes 149.1-149.3  Marc 14.26  Psaumes 95.1-95.2  
 3  Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu. 
2 Chroniques 8.13  Colossiens 2.16  Deutéronome 16.15  Nombres 10.1-10.10  1 Chroniques 16.42  
 4  Kwa maana ni sheria kwa Israeli, Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.  
5  Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua naliyasikia. 
Psaumes 114.1  Jérémie 5.15  Deutéronome 28.49  Psaumes 77.15  1 Corinthiens 14.21-14.22  
 6  Nimelitenga bega lake na mzigo, Mikono yake ikaachana na kikapu. 
Esaïe 9.4  Esaïe 10.27  Exode 6.6  Exode 1.14  Psaumes 68.13  
 7  Katika shida uliniita nikakuokoa; Nalikuitikia katika sitara ya radi; Nalikujaribu penye maji ya Meriba. 
Nombres 20.13  Exode 19.19  Psaumes 50.15  Exode 2.23  Exode 14.10  
 8  Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya, Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza; 
Psaumes 50.7  Jean 3.11  Deutéronome 32.46  Deutéronome 5.27  Actes 20.21  
 9  Usiwe na mungu mgeni ndani yako; Wala usimsujudie mungu mwingine. 
Esaïe 43.12  Deutéronome 32.12  Malachie 2.11  Exode 20.3-20.5  1 Corinthiens 8.5-8.6  
 10  Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza. 
Exode 20.2  Psaumes 37.3-37.4  Jérémie 11.4  Jean 16.23  Apocalypse 21.6  
 11  Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka. 
Exode 32.1  Deutéronome 32.15  Proverbes 1.30  Jérémie 7.23-7.24  Deutéronome 32.18  
 12  Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao. 
Romains 1.24  Jérémie 7.24  Actes 7.42  Romains 1.26-1.27  Esaïe 30.1  
 13  Laiti watu wangu wangenisikiliza, Na Israeli angeenenda katika njia zangu; 
Deutéronome 5.29  Esaïe 48.18  Matthieu 23.37  Luc 19.41-19.42  Deutéronome 10.12-10.13  
 14  Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu; 
Amos 1.8  Zacharie 13.7  Nombres 14.45  Josué 23.13  Juges 2.20-2.23  
 15  Wamchukiao Bwana wangenyenyekea mbele zake, Bali wakati wao ungedumu milele. 
Romains 1.30  Jean 15.22-15.23  Psaumes 63.3  Deutéronome 7.10  Exode 20.5  
 16  Naam, ningewalisha kwa unono wa ngano, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani. 
Psaumes 147.14  Deutéronome 32.13-32.14  Job 29.6  Juges 14.18  1 Samuel 14.25-14.26