Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 8.5
Bible en Swahili de l’est


1 Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;Psaumes 113.2-113.4 Psaumes 8.9 Psaumes 57.5 Psaumes 148.13 Hébreux 7.26
2 Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.Matthieu 21.16 1 Corinthiens 1.27 Psaumes 44.16 Matthieu 11.25 Psaumes 84.5-84.7
3 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;Psaumes 111.2 Psaumes 104.19 Genèse 1.1 Job 25.3 Psaumes 148.3
4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?Psaumes 144.3 Job 7.17 Hébreux 2.6-2.9 2 Chroniques 6.18 Job 25.6
5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;Hébreux 2.7 Hébreux 2.9 Genèse 1.26-1.27 Genèse 2.7 Psaumes 103.20
6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.Genèse 1.28 Genèse 1.26 Ephésiens 1.22 Matthieu 28.18 Hébreux 2.8
7 Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;Genèse 2.20
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.Genèse 1.20-1.25 Psaumes 148.10 Job 40.15-41.34 Job 38.39-39.30
9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!Psaumes 8.1 Deutéronome 33.26 Psaumes 104.24 Job 11.7

Cette Bible est dans le domaine public.