Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 64.2
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.Actes 18.9-18.10 Psaumes 27.7 Psaumes 34.4 Lamentations 3.55-3.56 Psaumes 140.1
2 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;Jérémie 11.19 Psaumes 56.6 Psaumes 27.5 Matthieu 26.3-26.4 Psaumes 109.2-109.3
3 Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,Psaumes 58.7 Psaumes 57.4 Psaumes 11.2 Proverbes 12.18 Jacques 3.6-3.8
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.Psaumes 55.19 Jean 19.6 Psaumes 11.2 1 Samuel 18.11 Psaumes 64.7
5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona?Psaumes 10.11 Psaumes 140.5 Psaumes 124.7 Psaumes 94.7 1 Samuel 23.19-23.23
6 Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili; Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao, Na moyo wake, huwa siri kabisa.Psaumes 35.11 Psaumes 49.11 Daniel 6.4-6.5 Jean 19.7 1 Samuel 24.9
7 Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha, Kwa mshale mara watapigwa.Psaumes 7.12-7.13 Esaïe 30.13 Lamentations 3.12-3.13 1 Chroniques 10.3-10.7 Deutéronome 32.42
8 Ndivyo watakavyokwazwa, Ulimi wao wenyewe ukishindana nao. Wote wawaonao watatikisa kichwa.Proverbes 18.7 Proverbes 12.13 Luc 19.22 Jérémie 18.16 Psaumes 22.7
9 Na watu wote wataogopa, Wataitangaza kazi ya Mungu, Na kuyafahamu matendo yake.Jérémie 51.10 Jérémie 50.28 Psaumes 40.3 Psaumes 119.20 Esaïe 5.12
10 Mwenye haki atamfurahia Bwana na kumkimbilia, Na wote wenye moyo wa adili watajisifu.Psaumes 58.10 Job 22.19 Psaumes 25.20 Psaumes 112.2 Psaumes 97.11

Cette Bible est dans le domaine public.