Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 29.6
Bible en Swahili de l’est


1 Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu;Psaumes 96.7-96.9 Psaumes 68.31-68.34 1 Chroniques 16.28-16.29 Esaïe 60.12 Apocalypse 5.11-5.14
2 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.2 Chroniques 20.21 Psaumes 110.3 Psaumes 96.8-96.9 Psaumes 90.17 Psaumes 97.9
3 Sauti ya Bwana i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; Bwana yu juu ya maji mengi.Psaumes 18.13-18.15 Psaumes 93.3-93.4 Psaumes 24.7-24.10 Apocalypse 16.18 Apocalypse 17.14-17.15
4 Sauti ya Bwana ina nguvu; Sauti ya Bwana ina adhama;Psaumes 68.33 Job 26.11-26.14 Luc 8.25 Job 40.9-40.12 Ezéchiel 10.5
5 Sauti ya Bwana yaivunja mierezi; Naam, Bwana aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni;Juges 9.15 Esaïe 2.13 Psaumes 104.16
6 Airusha-rusha kama ndama wa ng’ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati.Deutéronome 3.9 Nombres 23.22 Habakuk 3.6-3.11 Psaumes 114.4-114.7 Apocalypse 20.11
7 Sauti ya Bwana yaipasua miali ya moto;Psaumes 77.18 Nombres 16.35 Lévitique 10.2 2 Rois 1.10-1.12 Job 37.3
8 Sauti ya Bwana yalitetemesha jangwa; Bwana alitetemesha jangwa la Kadeshi.Nombres 13.26 Job 9.6 Aggée 2.6 Psaumes 46.3 Psaumes 18.7
9 Sauti ya Bwana yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu.Job 39.1-39.3 Psaumes 46.2-46.5 Psaumes 48.9 Esaïe 9.18 Psaumes 135.1-135.2
10 Bwana aliketi juu ya Gharika; Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele.Psaumes 10.16 Genèse 6.17 Psaumes 2.6-2.9 Genèse 8.1-8.2 Matthieu 6.13
11 Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.Nombres 6.24-6.27 Esaïe 40.31 Esaïe 41.10 Esaïe 40.29 Psaumes 68.35

Cette Bible est dans le domaine public.