Certitude de l’exaucement
1 Ee Bwana, nitakuita Wewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Psaumes 18.2 Psaumes 83.1 Psaumes 143.7 Proverbes 1.12 Psaumes 35.22
2 Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo, Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.
Psaumes 5.7 Psaumes 138.2 Psaumes 141.2 Psaumes 134.2 1 Timothée 2.8
3 Usinikokote pamoja na wasio haki, Wala pamoja na watenda maovu. Wawaambiao jirani zao maneno ya amani, Lakini mioyoni mwao mna madhara.Psaumes 12.2 Psaumes 55.21 Psaumes 26.9 Psaumes 62.4 Matthieu 25.41
4 Uwape sawasawa na vitendo vyao, Na kwa kadiri ya ubaya wa kufanya kwao, Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao, Uwalipe stahili zao.
2 Timothée 4.14 Apocalypse 18.6 Psaumes 62.12 Ezéchiel 38.10 Romains 11.22
5 Maana hawazifahamu kazi za Bwana, Wala matendo ya mikono yake. Atawavunja wala hatawajenga;
Esaïe 5.12 Esaïe 22.11 Romains 1.20 2 Samuel 7.13 Esaïe 26.9-26.11
6 Na ahimidiwe Bwana. Maana ameisikia sauti ya dua yangu;
Psaumes 66.19-66.20 Psaumes 116.1-116.2 Psaumes 31.21-31.22 Psaumes 69.33-69.34 Psaumes 107.19-107.22
7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
Psaumes 13.5 Esaïe 61.10 Psaumes 30.11-30.12 Psaumes 69.30 Psaumes 56.3-56.4
8 Bwana ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.
Psaumes 20.6 1 Samuel 16.13 Esaïe 61.1 Psaumes 140.7 Psaumes 2.2
9 Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge, uwachukue milele.
Esaïe 40.11 Deutéronome 9.29 Psaumes 78.71 Esdras 1.4 1 Rois 8.51