Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 29 Bible en Swahili de l’est
La toute-puissance de Dieu
1 Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu; 2 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu. 3 Sauti ya Bwana i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; Bwana yu juu ya maji mengi. 4 Sauti ya Bwana ina nguvu; Sauti ya Bwana ina adhama; 5 Sauti ya Bwana yaivunja mierezi; Naam, Bwana aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni; 6 Airusha-rusha kama ndama wa ng’ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati. 7 Sauti ya Bwana yaipasua miali ya moto; 8 Sauti ya Bwana yalitetemesha jangwa; Bwana alitetemesha jangwa la Kadeshi. 9 Sauti ya Bwana yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu. 10 Bwana aliketi juu ya Gharika; Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele. 11 Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.