1  Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa? 
Psaumes 39.4  Job 14.5-14.6  Job 14.13-14.14  Lévitique 25.50  Ecclésiaste 8.8  
 2  Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake; 
Lévitique 19.13  Jérémie 6.4  Deutéronome 24.15  Jacques 5.4  Malachie 3.5  
 3  Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha. 
Psaumes 6.6  Ecclésiaste 1.14  Job 16.7  Psaumes 39.5  Job 29.2  
 4  Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. 
Deutéronome 28.67  Job 7.13-7.14  Esaïe 54.11  Job 30.17  Psaumes 6.6  
 5  Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena. 
Job 17.14  Esaïe 14.11  Job 2.7-2.8  Job 24.20  Esaïe 1.6  
 6  Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini. 
Job 9.25  Job 17.15  Job 17.11  Esaïe 38.12-38.13  1 Pierre 1.24  
 7  Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena. 
Psaumes 78.39  Jacques 4.14  Job 10.21-10.22  Jérémie 15.15  Psaumes 89.47  
 8  Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena; Macho yako yatanielekea, lakini sitakuwapo. 
Job 20.9  Psaumes 37.36  Job 8.18  Job 13.27  Psaumes 39.11  
 9  Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa. 
2 Samuel 12.23  Job 16.22  Job 14.10-14.14  Job 30.15  Job 10.21  
 10  Hatarudi tena nyumbani kwake, Wala mahali pake hapatamjua tena. 
Job 8.18  Psaumes 103.16  Job 20.9  Job 27.23  Job 27.21  
 11  Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu. 
Psaumes 40.9  Job 10.1  1 Samuel 1.10  Esaïe 38.15  Job 21.25  
 12  Je! Mimi ni bahari, au je! Ni nyangumi? Hata ukawaweka walinzi juu yangu? 
Job 38.6-38.11  Ezéchiel 32.2-32.3  Job 41.1-41.34  Lamentations 3.7  Job 7.17  
 13  Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituza moyo, Malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu; 
Psaumes 6.6  Job 9.27-9.28  Job 7.3-7.4  Psaumes 77.4  
 14  Ndipo unitishapo kwa ndoto, Na kunitia hofu kwa maono; 
Daniel 2.1  Genèse 41.8  Juges 7.13-7.14  Matthieu 27.19  Genèse 40.5-40.7  
 15  Hata nafsi yangu huchagua kunyongwa, Na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya. 
2 Samuel 17.23  Matthieu 27.5  
 16  Ninadhoofika; sitaishi sikuzote; Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio. 
Job 10.1  1 Rois 19.4  Job 10.20  Job 6.9  Job 14.6  
 17  Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza, Na kumtia moyoni mwako, 
Hébreux 2.6  Psaumes 8.4  Psaumes 144.3  1 Samuel 24.14  Job 34.14-34.15  
 18  Na kumwangalia kila asubuhi, Na kumjaribu kila dakika? 
1 Pierre 1.7  Exode 20.5  Esaïe 38.12-38.13  Genèse 22.1  Deutéronome 8.16  
 19  Je! Hata lini hukomi kuniangalia; Wala kunisumbua hata nimeze mate? 
Job 9.18  Job 14.6  Psaumes 94.3  Psaumes 13.1-13.3  Apocalypse 6.10  
 20  Kwamba nimefanya dhambi, nikufanyieje Ee mlinda wanadamu? Mbona umeniweka niwe shabaha yako, Hata nimekuwa mzigo kwa nafsi yangu? 
Lamentations 3.12  Psaumes 36.6  Job 16.12-16.14  Psaumes 80.4  Job 35.6  
 21  Nawe, je! Mbona hunisamehe makosa yangu, Na kuniondolea maovu yangu? Kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; Nawe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwapo. 
Job 10.14  Daniel 12.2  Lamentations 5.20-5.22  Esaïe 64.9  Job 17.14