Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 23.9
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Hata leo mashitaka yangu yana uchungu; Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu.Job 10.1 Lamentations 3.19-3.20 Psaumes 77.2-77.9 Job 11.6 Psaumes 32.4
3 Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona, Nifike hata hapo anapokaa!Job 16.21 Job 13.3 Esaïe 55.6-55.7 2 Corinthiens 5.19-5.20 Job 40.1-40.5
4 Ningeiweka daawa yangu mbele yake, Na kukijaza kinywa changu hoja.Job 13.18 Josué 7.8-7.9 Job 37.19 Psaumes 43.1 Genèse 18.25-18.32
5 Ningeyajua maneno atakayonijibu, Na kuelewa na hayo atakayoniambia.1 Corinthiens 4.3-4.4 Job 13.22-13.23 Job 10.2 Job 42.2-42.6
6 Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake? La, lakini angenisikiliza.Job 13.21 Psaumes 138.3 Job 9.19 Ezéchiel 20.35 Ezéchiel 20.33
7 Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.Job 13.3 Romains 8.1 Job 9.15 Romains 3.19-3.22 Esaïe 1.18
8 Tazama, naenda mbele, wala hayuko; Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;Job 9.11 Psaumes 10.1 Job 35.14 1 Timothée 6.16 Psaumes 13.1-13.3
9 Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.Psaumes 89.46 Esaïe 8.17
10 Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.1 Pierre 1.7 Psaumes 139.1-139.3 Psaumes 66.10 Jacques 1.12 Zacharie 13.9
11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.Psaumes 44.18 Psaumes 17.5 Psaumes 125.5 Romains 2.7 2 Pierre 2.20-2.22
12 Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,Jean 4.34 Jérémie 15.16 Psaumes 119.103 Job 22.22 Jean 6.66-6.69
13 Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza? Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.Psaumes 115.3 Daniel 4.35 Job 12.14 Nombres 23.19-23.20 Proverbes 19.21
14 Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa; Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.1 Thessaloniciens 3.3 Psaumes 97.2 Michée 6.9 Psaumes 77.19 Esaïe 40.27-40.28
15 Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake; Nitakapofikiri, namwogopa.Psaumes 119.120 Job 23.3 Habakuk 3.16 Job 31.23 Job 10.15
16 Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia, Naye Mwenyezi amenitaabisha;Psaumes 22.14 Job 27.2 Deutéronome 20.3 Jérémie 51.46 Esaïe 6.5
17 Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza, Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.Job 19.8 Job 18.18 2 Rois 22.20 Job 6.9 Job 22.11

Cette Bible est dans le domaine public.