Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 23.7
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Hata leo mashitaka yangu yana uchungu; Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu.Job 10.1 Job 7.11 Job 6.2-6.3 Lamentations 3.19-3.20 Psaumes 77.2-77.9
3 Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona, Nifike hata hapo anapokaa!Job 16.21 Job 13.3 Job 31.35-31.37 Jérémie 14.7 Esaïe 55.6-55.7
4 Ningeiweka daawa yangu mbele yake, Na kukijaza kinywa changu hoja.Job 13.18 Genèse 32.12 Exode 32.12-32.13 Josué 7.8-7.9 Job 37.19
5 Ningeyajua maneno atakayonijibu, Na kuelewa na hayo atakayoniambia.Job 42.2-42.6 1 Corinthiens 4.3-4.4 Job 13.22-13.23 Job 10.2
6 Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake? La, lakini angenisikiliza.Job 13.21 Esaïe 27.8 Psaumes 138.3 Job 9.19 Ezéchiel 20.35
7 Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.Job 13.3 Jérémie 3.5 Romains 8.33-8.34 Romains 8.1 Job 9.15
8 Tazama, naenda mbele, wala hayuko; Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;Job 9.11 Psaumes 10.1 Job 35.14 1 Timothée 6.16 Esaïe 45.15
9 Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.Psaumes 89.46 Esaïe 8.17
10 Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.1 Pierre 1.7 Psaumes 139.1-139.3 Psaumes 66.10 Jacques 1.12 Zacharie 13.9
11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.Psaumes 44.18 Psaumes 17.5 Psaumes 125.5 Romains 2.7 2 Pierre 2.20-2.22
12 Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,Jean 4.34 Jérémie 15.16 Psaumes 119.103 Job 22.22 Jean 6.66-6.69
13 Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza? Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.Psaumes 115.3 Daniel 4.35 Job 12.14 Nombres 23.19-23.20 Proverbes 19.21
14 Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa; Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.1 Thessaloniciens 3.3 1 Pierre 2.8 1 Thessaloniciens 5.9 Psaumes 97.2 Michée 6.9
15 Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake; Nitakapofikiri, namwogopa.Psaumes 119.120 Job 10.15 Psaumes 77.3 Job 23.3 Habakuk 3.16
16 Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia, Naye Mwenyezi amenitaabisha;Psaumes 22.14 Job 27.2 Deutéronome 20.3 Joël 1.15 Jérémie 51.46
17 Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza, Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.Job 19.8 Esaïe 57.1 Job 18.6 Job 18.18 2 Rois 22.20

Cette Bible est dans le domaine public.