Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 10.2
Bible en Swahili de l’est


1 Basi Wafilisti wakapigana juu ya Israeli; nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima Gilboa.1 Samuel 31.1-31.13 1 Chroniques 10.8 2 Samuel 1.6 1 Samuel 28.1 1 Samuel 29.1-29.2
2 Nao Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe; Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli.Esaïe 57.1-57.2 1 Chroniques 9.39 2 Rois 25.7 1 Samuel 14.49 Exode 20.5
3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde.Genèse 49.23-49.24 1 Samuel 31.3-31.6 2 Samuel 1.4-1.10 Amos 2.14
4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao, wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.1 Samuel 31.4 1 Samuel 17.26 Matthieu 27.4-27.5 2 Samuel 1.14-1.16 1 Rois 16.18
5 Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa. 6 Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu; na nyumba yake yote wakafa pamoja.1 Samuel 4.10-4.11 Ecclésiaste 9.1-9.2 Osée 13.10-13.11 1 Samuel 12.25 1 Samuel 4.18
7 Kisha watu wote wa Israeli, waliokuwa huko bondeni, walipoona ya kuwa wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.Juges 6.2 Deutéronome 28.43 1 Samuel 13.6 Lévitique 26.31 1 Samuel 31.7
8 Hata ikawa siku ya pili yake Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara hao waliouawa, walimwona Sauli na wanawe wameanguka juu ya mlima Gilboa.2 Chroniques 20.25 2 Rois 3.23 1 Samuel 31.8
9 Wakamvua mavazi, wakamtwalia kichwa, na silaha zake, kisha wakapeleka wajumbe kwenda nchi ya Wafilisti pande zote, ili kutangaza habari kwa sanamu zao, na kwa watu.1 Samuel 31.9-31.10 Daniel 5.2-5.4 2 Samuel 1.20 Juges 16.23-16.24 Matthieu 14.11
10 Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa miungu yao, wakakikaza kichwa chake nyumbani mwa Dagoni.1 Samuel 31.10 1 Samuel 5.2-5.7
11 Na watu wote wa Yabesh-gileadi waliposikia hayo yote Wafilisti waliyomtenda Sauli,1 Samuel 31.11-31.13 1 Samuel 11.1-11.11 2 Samuel 2.4-2.7
12 wakainuka mashujaa wote, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi, wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga muda wa siku saba.2 Samuel 3.35 Genèse 35.8 2 Samuel 21.12-21.14 Genèse 50.10
13 Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,Lévitique 20.6 1 Samuel 15.23 Lévitique 19.31 Esaïe 8.19 Deutéronome 18.10-18.14
14 asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.1 Samuel 15.28 1 Samuel 13.14 2 Samuel 3.9-3.10 1 Chroniques 12.23 1 Samuel 28.17

Cette Bible est dans le domaine public.