Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 6.2
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.Deutéronome 7.3-7.4 Malachie 2.11 Esdras 9.12 Romains 9.7-9.8 Esdras 9.1-9.2
3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.Néhémie 9.30 Psaumes 78.39 1 Pierre 3.18-3.20 Esaïe 63.10 Nombres 11.17
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.Nombres 13.33 2 Samuel 21.15-21.22 Deutéronome 2.20-2.21 Deutéronome 3.11 1 Samuel 17.4
5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.Matthieu 15.19 Genèse 8.21 Romains 1.28-1.31 Marc 7.21-7.23 Jérémie 17.9
6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.1 Samuel 15.11 Esaïe 63.10 Ephésiens 4.30 1 Samuel 15.29 Nombres 23.19
7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.Proverbes 16.4 Romains 3.20-3.22 Psaumes 24.1-24.2 Sophonie 1.3 Osée 4.3
8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.Genèse 19.19 Luc 1.30 Exode 33.12-33.17 Proverbes 3.4 2 Timothée 1.18
9 Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.Luc 1.6 2 Pierre 2.5 Genèse 5.24 Genèse 7.1 Hébreux 11.7
10 Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi.Genèse 5.32
11 Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.Ezéchiel 8.17 Genèse 10.9 Osée 4.1-4.2 Luc 1.6 Psaumes 140.11
12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.Psaumes 53.2-53.3 Job 33.27 Job 22.15-22.17 Genèse 9.12 Genèse 7.1
13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.1 Pierre 4.7 Genèse 49.5 Hébreux 11.7 Jérémie 51.13 Jérémie 4.23-4.28
14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.Matthieu 24.38 Exode 2.3 1 Pierre 3.20 Luc 17.27
15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; mikono mia tatu urefu wa safina, mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake.Genèse 7.20 Deutéronome 3.11
16 Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu.Luc 13.25 Genèse 8.6 Ezéchiel 41.16 Ezéchiel 42.3 2 Samuel 6.16
17 Na tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.2 Pierre 2.5 Genèse 7.4 Genèse 7.21-7.23 Psaumes 29.10 1 Pierre 3.20
18 Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe.Genèse 7.7 Genèse 7.13 Genèse 7.1 Genèse 17.7 Genèse 17.21
19 Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, kuwahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke.Genèse 7.8-7.9 Genèse 7.2-7.3 Psaumes 36.6 Genèse 8.17 Genèse 7.15-7.16
20 Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna watakuja kwako ili uwahifadhi.Jean 5.40 Genèse 7.8-7.16 Genèse 2.19 Genèse 1.28 Actes 10.11-10.12
21 Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao.Genèse 1.29-1.30 Psaumes 35.6 Psaumes 147.9 Psaumes 104.27-104.28 Job 38.41
22 Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.Genèse 7.5 Hébreux 11.7-11.8 Matthieu 7.24-7.27 Exode 40.23 Genèse 7.9

Cette Bible est dans le domaine public.