Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 32.18
Bible en Swahili de l’est


1 Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye.
Psaumes 91.11 Psaumes 34.7 1 Corinthiens 3.22 Ephésiens 3.10 2 Rois 6.16-6.17

Préparatifs de la rencontre avec Ésaü

2 Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu.
2 Samuel 2.8 Josué 21.38 Luc 2.13 Psaumes 148.2 1 Rois 2.8
3 Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.
Genèse 25.30 Josué 24.4 Deutéronome 2.5 Genèse 33.14 Genèse 14.6
4 Akawaagiza akisema, Mwambieni hivi bwana wangu, Esau, Hivi ndivyo asemavyo mtumwa wako, Yakobo; Nimekaa ugenini kwa Labani, na kukawia huko hata sasa,
Luc 14.11 Genèse 32.18 1 Pierre 3.6 Ecclésiaste 10.4 Genèse 33.8
5 nami nina ng’ombe, na punda, na kondoo, na watumwa, na vijakazi; nami nimepeleka watu nimpashe bwana wangu habari, nipate neema machoni pako.
Genèse 33.8 Genèse 33.15 1 Samuel 1.18 Genèse 33.11 2 Samuel 16.4
6 Wale wajumbe wakarudi kwa Yakobo wakisema, Tulifika kwa ndugu yako, Esau, naye anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye.
Genèse 33.1 Genèse 32.8 Genèse 32.11 Genèse 27.40-27.41 Amos 5.19
7 Ndipo Yakobo akaogopa sana, na kufadhaika sana, akawagawanya watu waliopo pamoja naye, na kondoo, na ng’ombe, na ngamia, wawe matuo mawili.
Genèse 35.3 Psaumes 61.2 Psaumes 142.4 Psaumes 31.13 Esaïe 28.26
8 Akasema, Akija Esau kwa kundi la kwanza, akalipiga, kundi litakalosalia litaokoka.
Matthieu 10.16 Genèse 33.1-33.3
9 Yakobo akasema, Ee Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Bwana, uliyeniambia, Rudi uende mpaka nchi yako, na kwa jamaa zako, nami nitakutendea mema;
Genèse 31.42 Genèse 28.13 Genèse 31.13 Genèse 31.3 Genèse 31.53
10 mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nalivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa matuo mawili.
Genèse 24.27 Psaumes 18.35 2 Samuel 7.18 1 Timothée 1.12-1.15 Michée 7.20
11 Uniokoe sasa na mkono wa ndugu yangu, mkono wa Esau, maana mimi namwogopa, asije akanipiga, na mama pamoja na wana.
Psaumes 59.1-59.2 Proverbes 18.19 Psaumes 31.2 Daniel 3.17 Psaumes 16.1
12 Nawe ulisema, Hakika nitakutendea mema, nami nitafanya uzao wako uwe kama mchanga wa bahari, usiohesabika kwa kuwa mwingi.
Genèse 28.13-28.15 Nombres 23.19 Tite 1.2 2 Timothée 2.13 Genèse 46.3-46.4
13 Akakaa huko usiku ule. Kisha akatwaa baadhi ya vitu alivyokuwa navyo, kuwa zawadi kwa Esau, nduguye;
Genèse 43.11 Proverbes 18.16 Genèse 43.26 Proverbes 17.8 Proverbes 21.14
14 mbuzi wake mia mbili, na mbuzi waume ishirini, kondoo wake mia mbili, na kondoo waume ishirini;
Deutéronome 8.18 Genèse 31.16 Job 1.3 Genèse 30.43 Genèse 31.9
15 ngamia wanyonyeshao thelathini pamoja na wana wao, ng’ombe wake arobaini na mafahali kumi; punda wake ishirini na wana wao kumi.
16 Akawatia mkononi mwa watumwa wake, kila kundi peke yake. Naye akawaambia watumwa wake, Vukeni mbele yangu, mkaache nafasi kati ya kundi na kundi.
Matthieu 10.16 Psaumes 112.5 Genèse 32.20 Esaïe 28.26 Proverbes 2.11
17 Akamwagiza yule wa kwanza akasema, Esau, ndugu yangu, akikukuta, na kukuuliza, akisema, Wewe u wa nani? Unakwenda wapi? Tena ni wa nani hawa walio mbele yako?
Genèse 33.3
18 Basi, useme, Ni wa mtumwa wako, Yakobo, ni zawadi, aliyompelekea bwana wangu, Esau. Na tazama, yeye mwenyewe yuko nyuma yetu.
Genèse 32.4-32.5
19 Akamwagiza tena wa pili, na wa tatu, wote waliofuata makundi, akisema, Hivi ndivyo mtakavyomwambia Esau, akiwakuta.
20 Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu.
Job 42.8-42.9 Proverbes 21.14 1 Samuel 6.5 1 Samuel 25.17-25.35 Proverbes 15.18
21 Basi ile zawadi ikavuka mbele yake, naye mwenyewe akakaa usiku ule kambini.
22 Akaondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki.
Deutéronome 3.16 Josué 12.2 Deutéronome 2.37 1 Timothée 5.8 Genèse 35.22-35.26
23 Akawatwaa, akawavusha mto, akavusha na vyote alivyokuwa navyo.
24 Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
Osée 12.3-12.5 Genèse 32.30 Genèse 32.28 Luc 13.24 Ephésiens 6.12

Jacob à Peniel

25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
Osée 12.3-12.4 2 Corinthiens 12.7-12.9 Genèse 32.32 Esaïe 45.11 Matthieu 15.22-15.28
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
Osée 12.4 Psaumes 115.12-115.13 Luc 18.1-18.7 Psaumes 67.1 1 Chroniques 4.10
27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Genèse 35.10 2 Rois 17.34 Genèse 17.5 Apocalypse 2.17 Genèse 33.4
29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
Juges 13.16-13.18 Job 11.7 Osée 6.1 Luc 1.19 Genèse 28.13-28.14
30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.
Genèse 16.13 Nombres 12.8 Esaïe 6.5 Exode 24.10-24.11 Deutéronome 5.24
31 Jua likamzukia akivuka Penueli, akachechemea kwa sababu ya paja la mguu wake.
2 Corinthiens 12.9 Genèse 19.15 Malachie 4.2 Genèse 32.25 Juges 8.8
32 Kwa hiyo wana wa Israeli hawali ule mshipa ulio katika uvungu wa paja hata leo; maana alimgusa Yakobo panapo uvungu wa paja katika mshipa wa kiuno.
1 Samuel 5.5

Cette Bible est dans le domaine public.