Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Thessaloniciens 4.7
Bible en Swahili de l’est


1 Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.Colossiens 1.10 2 Thessaloniciens 1.3 Philippiens 1.9 Ephésiens 4.1 2 Pierre 3.18
2 Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.Ezéchiel 3.17 Matthieu 28.20 1 Corinthiens 9.21 2 Thessaloniciens 3.10 2 Thessaloniciens 3.6
3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;1 Pierre 4.2 1 Thessaloniciens 5.23 Colossiens 3.5 Ephésiens 5.17 Romains 12.2
4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;1 Corinthiens 7.9 1 Pierre 3.7 Hébreux 13.4 1 Corinthiens 7.2 1 Corinthiens 6.15
5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.Galates 4.8 Romains 1.26 2 Thessaloniciens 1.8 Actes 17.30-17.31 Ephésiens 2.12
6 Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.Romains 12.19 Hébreux 13.4 Ephésiens 4.28 Luc 12.5 Jacques 2.6
7 Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.Ephésiens 1.4 Lévitique 11.44 1 Thessaloniciens 2.3 Hébreux 12.14 Galates 5.19
8 Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.1 Jean 3.24 Luc 10.16 1 Samuel 8.7 Néhémie 9.30 Jean 12.48
9 Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.1 Jean 3.11 Romains 12.10 1 Jean 3.23 Hébreux 13.1 1 Thessaloniciens 5.1
10 Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana.1 Thessaloniciens 3.12 1 Thessaloniciens 1.7 2 Thessaloniciens 1.3 Philippiens 3.13-3.15 Philippiens 1.9
11 Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;Ephésiens 4.28 1 Pierre 4.15 1 Pierre 3.4 Ecclésiaste 4.6 1 Timothée 2.2
12 ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.Marc 4.11 Colossiens 4.5 Romains 13.13 1 Timothée 3.7 Romains 12.17
13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.Ephésiens 2.12 2 Pierre 3.4 Daniel 12.2 Jean 11.11-11.13 Actes 7.60
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.Romains 8.11 2 Corinthiens 4.13-4.14 Apocalypse 1.18 1 Thessaloniciens 4.13 Matthieu 24.31
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.1 Corinthiens 15.51-15.53 2 Corinthiens 4.14 Psaumes 119.147-119.148 Matthieu 17.25 Psaumes 88.13
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.Apocalypse 1.7 Matthieu 24.30-24.31 Matthieu 16.27 1 Corinthiens 15.51-15.52 2 Thessaloniciens 1.7
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.Apocalypse 11.12 1 Corinthiens 15.52 Jean 14.3 Jean 12.26 Apocalypse 7.14-7.17
18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.1 Thessaloniciens 5.14 1 Thessaloniciens 5.11 Hébreux 10.24-10.25 Luc 21.28 Hébreux 12.12

Cette Bible est dans le domaine public.