Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Thessaloniciens 4.3
Bible en Swahili de l’est


1 Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.Colossiens 1.10 2 Thessaloniciens 1.3 Philippiens 1.9 Hébreux 13.16 2 Thessaloniciens 2.1
2 Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.Matthieu 28.20 Ezéchiel 3.17 1 Corinthiens 9.21 2 Thessaloniciens 3.10 2 Thessaloniciens 3.6
3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;1 Pierre 4.2 1 Thessaloniciens 5.23 Colossiens 3.5 Ephésiens 5.17 1 Thessaloniciens 4.4
4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;1 Corinthiens 7.9 1 Pierre 3.7 Romains 12.1 Hébreux 13.4 1 Corinthiens 7.2
5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.Galates 4.8 Romains 1.26 Actes 17.30-17.31 2 Thessaloniciens 1.8 Actes 17.23
6 Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.Romains 12.19 Hébreux 13.4 Ephésiens 4.28 Lévitique 25.14 Deutéronome 24.7
7 Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.Ephésiens 1.4 Lévitique 11.44 1 Thessaloniciens 2.3 Ephésiens 4.19 2 Thessaloniciens 2.13-2.14
8 Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.1 Jean 3.24 Luc 10.16 1 Samuel 8.7 Jean 12.48 Romains 5.5
9 Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.1 Jean 3.11 Romains 12.10 1 Jean 3.23 1 Thessaloniciens 5.1 Hébreux 13.1
10 Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana.1 Thessaloniciens 3.12 1 Thessaloniciens 1.7 2 Thessaloniciens 1.3 2 Corinthiens 8.1-8.2 Philippiens 3.13-3.15
11 Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;Ephésiens 4.28 1 Pierre 4.15 1 Pierre 3.4 1 Timothée 2.2 Tite 3.14
12 ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.Marc 4.11 Colossiens 4.5 Romains 13.13 Romains 12.17 1 Pierre 2.12
13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.Ephésiens 2.12 2 Pierre 3.4 Jean 11.11-11.13 Actes 7.60 Ezéchiel 37.11
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.Romains 8.11 2 Corinthiens 4.13-4.14 Apocalypse 1.18 1 Thessaloniciens 4.13 1 Thessaloniciens 3.13
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.1 Corinthiens 15.51-15.53 2 Corinthiens 4.14 Psaumes 88.13 1 Rois 20.35 1 Thessaloniciens 2.19
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.Apocalypse 1.7 Matthieu 24.30-24.31 Matthieu 16.27 1 Corinthiens 15.51-15.52 2 Thessaloniciens 1.7
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.Apocalypse 11.12 1 Corinthiens 15.52 Jean 14.3 Jean 12.26 Apocalypse 7.14-7.17
18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.1 Thessaloniciens 5.14 1 Thessaloniciens 5.11 Hébreux 10.24-10.25 Luc 21.28 Hébreux 12.12

Cette Bible est dans le domaine public.