1  Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. 
Colossiens 1.10  2 Thessaloniciens 1.3  Philippiens 1.9  Hébreux 13.16  2 Thessaloniciens 2.1  
 2  Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. 
Matthieu 28.20  Ezéchiel 3.17  1 Corinthiens 9.21  2 Thessaloniciens 3.10  2 Thessaloniciens 3.6  
 3  Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 
1 Pierre 4.2  1 Thessaloniciens 5.23  Colossiens 3.5  Ephésiens 5.17  1 Thessaloniciens 4.4  
 4  kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 
1 Corinthiens 7.9  1 Pierre 3.7  Romains 12.1  Hébreux 13.4  1 Corinthiens 7.2  
 5  si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. 
Galates 4.8  Romains 1.26  Actes 17.30-17.31  2 Thessaloniciens 1.8  Colossiens 3.5  
 6  Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. 
Romains 12.19  Hébreux 13.4  Ephésiens 4.28  Proverbes 22.22-22.23  Esaïe 5.7  
 7  Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. 
Lévitique 11.44  Ephésiens 1.4  1 Thessaloniciens 2.3  2 Thessaloniciens 2.13-2.14  Romains 8.29-8.30  
 8  Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu. 
1 Jean 3.24  Luc 10.16  1 Samuel 8.7  Romains 5.5  Néhémie 9.30  
 9  Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana. 
1 Jean 3.11  Romains 12.10  1 Jean 3.23  1 Thessaloniciens 5.1  Hébreux 13.1  
 10  Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana. 
1 Thessaloniciens 3.12  2 Thessaloniciens 1.3  1 Thessaloniciens 1.7  2 Corinthiens 8.1-8.2  Philippiens 3.13-3.15  
 11  Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; 
Ephésiens 4.28  1 Pierre 4.15  1 Pierre 3.4  1 Timothée 2.2  Tite 3.14  
 12  ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote. 
Marc 4.11  Colossiens 4.5  Romains 13.13  1 Pierre 2.12  1 Timothée 3.7  
 13  Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 
Ephésiens 2.12  2 Pierre 3.4  Ezéchiel 37.11  Daniel 12.2  Jean 11.11-11.13  
 14  Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 
Romains 8.11  2 Corinthiens 4.13-4.14  Apocalypse 1.18  1 Thessaloniciens 4.13  1 Thessaloniciens 3.13  
 15  Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 
1 Corinthiens 15.51-15.53  2 Corinthiens 4.14  Psaumes 88.13  1 Rois 20.35  1 Thessaloniciens 2.19  
 16  Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 
Apocalypse 1.7  Matthieu 24.30-24.31  Matthieu 16.27  1 Corinthiens 15.51-15.52  2 Thessaloniciens 1.7  
 17  Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 
Apocalypse 11.12  1 Corinthiens 15.52  Jean 14.3  Apocalypse 7.14-7.17  Jean 12.26  
 18  Basi, farijianeni kwa maneno hayo. 
1 Thessaloniciens 5.14  1 Thessaloniciens 5.11  Hébreux 10.24-10.25  Luc 21.28  Hébreux 12.12