Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Michée 5.7
Bible en Swahili de l’est


1 Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.Lamentations 3.30 Job 16.10 Esaïe 33.22 2 Rois 25.1-25.3 Ezéchiel 24.2
2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.Matthieu 2.6 Jean 7.42 Esaïe 11.1 Zacharie 9.9 Esaïe 9.6-9.7
3 Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli.Osée 11.8 Esaïe 10.20-10.21 Michée 4.7 Michée 4.9-4.10 Michée 7.13
4 Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za Bwana, kwa enzi ya jina la Bwana, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia.Michée 7.14 Luc 1.32 Zacharie 9.10 Psaumes 72.8 Esaïe 52.10
5 Na mtu huyu atakuwa amani yetu; wakati Mwashuri atakapoingia katika nchi yetu, na kuyakanyaga majumba yetu, hapo mtaondokesha wachungaji saba juu yake, na wakuu wanane.Zacharie 9.10 Luc 2.14 Ephésiens 2.14-2.17 Zacharie 9.13 Psaumes 72.7
6 Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.Esaïe 14.25 Genèse 10.8-10.11 2 Rois 17.3-17.5 Nahum 2.11-3.3 2 Rois 18.9-18.15
7 Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa Bwana, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu.Deutéronome 32.2 Michée 5.3 Psaumes 72.6 Osée 14.5 Esaïe 44.3
8 Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwana-simba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyaga-kanyaga na kurarua-rarua, wala hakuna wa kuokoa.Michée 4.13 Psaumes 50.22 Zacharie 10.5 Esaïe 41.15-41.16 Osée 5.14
9 Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.Esaïe 26.11 Psaumes 21.8 Esaïe 33.10 Esaïe 1.25 Psaumes 10.12
10 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana, nitawakatilia mbali farasi zako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;Zacharie 9.10 Osée 14.3 Esaïe 2.7 Jérémie 3.23 Psaumes 33.16-33.17
11 nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako zote nitaziangusha;Esaïe 2.12-2.17 Osée 10.14 Esaïe 6.11 Zacharie 4.6 Amos 5.9
12 nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana;Deutéronome 18.10-18.12 Apocalypse 22.15 Esaïe 8.19-8.20 Zacharie 13.2-13.4 Esaïe 27.9
13 nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako.Ezéchiel 6.9 Osée 2.16-2.17 Esaïe 17.7-17.8 Ezéchiel 36.25 Ezéchiel 37.23
14 Nami nitayang’oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako.Exode 34.13
15 Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu juu ya mataifa wasiosikiliza.2 Thessaloniciens 1.8 Michée 5.8 Psaumes 149.7 Esaïe 65.12

Cette Bible est dans le domaine public.