1  Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori. 
Osée 9.8  Osée 6.9  Osée 4.1  Juges 4.6  Malachie 2.1  
 2  Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi ndiye awakaripiaye wote pia. 
Osée 9.15  Esaïe 29.15  Osée 6.9  Esaïe 1.5  Jérémie 18.18  
 3  Mimi namjua Efraimu, wala Israeli hakufichwa nisimwone; maana sasa, Ee Efraimu, umefanya uzinzi; Israeli ametiwa unajisi. 
Amos 3.2  Genèse 48.19-48.20  1 Rois 14.14-14.16  Osée 4.17-4.18  Osée 12.1  
 4  Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui Bwana. 
Osée 4.12  1 Jean 2.3-2.4  Jean 16.3  Jean 8.55  Psaumes 9.10  
 5  Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu watajikwaa katika uovu wao. Yuda naye atajikwaa pamoja nao. 
Osée 7.10  Ezéchiel 23.31-23.35  Amos 5.2  Matthieu 23.31  Luc 19.22  
 6  Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng’ombe wamtafute Bwana; lakini hawatamwona; amejitenga nao. 
Michée 6.6-6.7  Proverbes 1.28  Jean 7.34  Ezéchiel 8.6  Proverbes 15.8  
 7  Wametenda kwa hila juu ya Bwana; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawala pamoja na mashamba yao. 
Osée 6.7  Jérémie 3.20  Esaïe 48.8  Osée 2.11  Ezéchiel 12.28  
Punition d’Israël et Juda
 8  Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-Aveni; nyuma yako, Ee Benyamini! 
Osée 9.9  Osée 4.15  Joël 2.1  Jérémie 4.5  1 Samuel 15.34  
 9  Efraimu atakuwa ukiwa siku ya kukemewa; katika kabila za Israeli nimetangaza habari itakayotokea halafu bila shaka. 
Esaïe 46.10  Osée 9.11-9.17  Zacharie 1.6  Esaïe 28.1-28.4  Amos 3.7  
 10  Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji. 
Deutéronome 19.14  Deutéronome 27.17  Psaumes 32.6  Psaumes 93.3-93.4  Ezéchiel 7.8  
 11  Efraimu ameonewa, amesetwa katika hukumu, kwa sababu alikuwa radhi kufuata ubatili. 
Deutéronome 28.33  Michée 6.16  1 Rois 12.26-12.33  Amos 5.11-5.12  2 Rois 15.29  
 12  Kwa sababu hiyo mimi nimekuwa kama nondo kwa Efraimu, nimekuwa kama ubovu kwa nyumba ya Yuda. 
Esaïe 51.8  Job 13.28  Marc 9.43-9.48  Jonas 4.7  Esaïe 50.9  
 13  Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha yake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha yenu. 
Osée 7.11  Osée 12.1  Osée 10.6  Osée 8.9  Jérémie 30.12  
 14  Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwana-simba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukulia mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kupokonya. 
Michée 5.8  Psaumes 7.2  Osée 13.7-13.8  Esaïe 5.29  Psaumes 50.22  
 15  Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii. 
Esaïe 26.16  Psaumes 78.34  Jérémie 3.13  Psaumes 50.15  Jérémie 29.12-29.14