1  Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 
Luc 4.18-4.19  Luc 7.22  Esaïe 42.7  Matthieu 11.5  Psaumes 147.3  
 2  Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; 
Esaïe 34.8  Matthieu 5.4  Esaïe 57.18  Luc 4.19  Jérémie 31.13  
 3  kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. 
Jérémie 17.7-17.8  Esaïe 61.10  Psaumes 45.7  Jean 16.20  Psaumes 30.11  
 4  Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi. 
Esaïe 58.12  Esaïe 49.6-49.8  Ezéchiel 36.23-36.26  Ezéchiel 36.33-36.36  Amos 9.14-9.15  
 5  Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu. 
Esaïe 14.1-14.2  Esaïe 60.10-60.14  Ephésiens 2.12-2.20  
 6  Bali ninyi mtaitwa makuhani wa Bwana; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao. 
Exode 19.6  Esaïe 60.5-60.7  Esaïe 66.21  1 Pierre 2.9  1 Pierre 2.5  
 7  Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele. 
Esaïe 40.2  Zacharie 9.12  Psaumes 16.11  2 Thessaloniciens 2.16  Esaïe 60.19-60.20  
 8  Maana mimi, Bwana, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wivi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele. 
Esaïe 55.3  Psaumes 11.7  Genèse 17.7  Jérémie 32.40  Jérémie 7.8-7.11  
 9  Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika kabila za watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na Bwana. 
Esaïe 44.3  Psaumes 115.14  Zacharie 8.13  Romains 11.16-11.24  Genèse 22.18  
 10  Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu. 
Apocalypse 19.7-19.8  Apocalypse 21.2  Esaïe 49.18  Psaumes 132.16  Psaumes 132.9  
 11  Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote. 
Psaumes 85.11  Esaïe 60.18  Psaumes 72.3  Esaïe 62.7  Esaïe 58.11