Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 38.6
Bible en Swahili de l’est


1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.2 Samuel 17.23 2 Chroniques 32.24 Esaïe 38.1-38.8 2 Rois 20.1-20.11 Jean 11.1-11.5
2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana,Psaumes 50.15 Matthieu 6.6 1 Rois 8.30 Psaumes 91.15
3 akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.1 Chroniques 29.19 Psaumes 6.8 Néhémie 13.14 Psaumes 32.2 Psaumes 20.1-20.3
4 Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, 5 Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.2 Rois 18.2 Job 14.5 1 Rois 8.25 1 Jean 5.14-5.15 1 Rois 11.12-11.13
6 Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu.Esaïe 37.35 2 Timothée 4.17 Esaïe 31.4-31.5 Esaïe 12.6 2 Chroniques 32.22
7 Jambo hili liwe ishara kwako, itokayo kwa Bwana, ya kuwa Bwana atalitimiza jambo hili alilolisema;Juges 6.37-6.39 Esaïe 37.30 Esaïe 38.22 Esaïe 7.11-7.14 Genèse 9.13
8 Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.2 Chroniques 32.24 2 Rois 20.9-20.11 2 Chroniques 32.31 Josué 10.12-10.14 Matthieu 16.1
9 Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa hawezi, naye akapona ugonjwa wake.Psaumes 118.18-118.19 1 Samuel 2.1-2.10 Job 5.18 Jonas 2.1-2.9 Deutéronome 32.39
10 Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.2 Corinthiens 1.9 Psaumes 102.24 Job 7.7 Psaumes 107.18 Job 6.11
11 Nalisema, Sitamwona Bwana, yeye Bwana, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.Psaumes 27.13 Psaumes 6.4-6.5 Psaumes 116.8-116.9 Job 35.14-35.15 Psaumes 31.22
12 Kao langu limeondolewa kabisa, limechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.2 Corinthiens 5.1 Hébreux 1.12 Psaumes 73.14 Job 4.20 Psaumes 102.23-102.24
13 Nalijituliza hata asubuhi; kama simba, aivunja mifupa yangu yote; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.Psaumes 51.8 Daniel 6.24 Job 10.16-10.17 1 Rois 20.36 Job 16.12-16.14
14 Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Naliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee Bwana, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.Esaïe 59.11 Psaumes 69.3 Ezéchiel 7.16 Psaumes 119.122-119.123 Job 30.29
15 Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.1 Rois 21.27 Job 7.11 Job 10.1 Esdras 9.10 Job 21.25
16 Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi; Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote; Kwa hiyo uniponye na kunihuisha.Deutéronome 8.3 Hébreux 12.10-12.11 Matthieu 4.4 Psaumes 71.20 Psaumes 119.25
17 Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.Esaïe 43.25 Jérémie 31.34 Jonas 2.6 Psaumes 86.13 Psaumes 30.3
18 Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.Ecclésiaste 9.10 Psaumes 6.5 Psaumes 30.9 Nombres 16.33 Psaumes 88.10-88.11
19 Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto kweli yako.Deutéronome 6.7 Deutéronome 4.9 Psaumes 78.3-78.6 Deutéronome 11.19 Exode 12.26-12.27
20 Bwana yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa Bwana.Psaumes 27.5-27.6 Psaumes 116.17-116.19 Psaumes 150.4 Habakuk 3.19 Psaumes 116.2
21 Maana Isaya amesema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona.Marc 7.33 2 Rois 20.7-20.8 Jean 9.6
22 Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionyesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa Bwana?Psaumes 84.10-84.12 Psaumes 84.1-84.2 Jean 5.14 Psaumes 118.18-118.19 Psaumes 122.1

Cette Bible est dans le domaine public.