Maladie et guérison d’Ézéchias
 1  Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. 
2 Samuel 17.23  2 Chroniques 32.24  Esaïe 38.1-38.8  2 Rois 20.1-20.11  Jean 11.1-11.5  
 2  Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana, 
Psaumes 50.15  Matthieu 6.6  1 Rois 8.30  Psaumes 91.15  
 3  akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. 
1 Chroniques 29.19  Psaumes 6.8  Néhémie 13.14  Psaumes 32.2  Psaumes 20.1-20.3  
 4  Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema,  
5  Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano. 
2 Rois 18.2  Job 14.5  1 Rois 8.25  1 Jean 5.14-5.15  1 Rois 11.12-11.13  
 6  Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu. 
Esaïe 37.35  2 Timothée 4.17  Esaïe 31.4-31.5  Esaïe 12.6  2 Chroniques 32.22  
 7  Jambo hili liwe ishara kwako, itokayo kwa Bwana, ya kuwa Bwana atalitimiza jambo hili alilolisema; 
Juges 6.37-6.39  Esaïe 37.30  Esaïe 38.22  Esaïe 7.11-7.14  Genèse 9.13  
 8  Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka. 
2 Chroniques 32.24  2 Rois 20.9-20.11  2 Chroniques 32.31  Josué 10.12-10.14  Matthieu 16.1  
 9  Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa hawezi, naye akapona ugonjwa wake. 
Psaumes 118.18-118.19  1 Samuel 2.1-2.10  Job 5.18  Jonas 2.1-2.9  Deutéronome 32.39  
 10  Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu. 
2 Corinthiens 1.9  Psaumes 102.24  Job 7.7  Psaumes 107.18  Job 6.11  
 11  Nalisema, Sitamwona Bwana, yeye Bwana, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani. 
Psaumes 27.13  Psaumes 6.4-6.5  Psaumes 116.8-116.9  Job 35.14-35.15  Psaumes 31.22  
 12  Kao langu limeondolewa kabisa, limechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza. 
2 Corinthiens 5.1  Hébreux 1.12  Psaumes 73.14  Job 4.20  Psaumes 102.23-102.24  
 13  Nalijituliza hata asubuhi; kama simba, aivunja mifupa yangu yote; Tangu mchana hata usiku wanimaliza. 
Psaumes 51.8  Daniel 6.24  Job 10.16-10.17  1 Rois 20.36  Job 16.12-16.14  
 14  Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Naliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee Bwana, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu. 
Esaïe 59.11  Psaumes 69.3  Ezéchiel 7.16  Psaumes 119.122-119.123  Job 30.29  
 15  Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu. 
1 Rois 21.27  Job 7.11  Job 10.1  Esdras 9.10  Job 21.25  
 16  Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi; Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote; Kwa hiyo uniponye na kunihuisha. 
Deutéronome 8.3  Hébreux 12.10-12.11  Matthieu 4.4  Psaumes 71.20  Psaumes 119.25  
 17  Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako. 
Esaïe 43.25  Jérémie 31.34  Jonas 2.6  Psaumes 86.13  Psaumes 30.3  
 18  Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako. 
Ecclésiaste 9.10  Psaumes 6.5  Psaumes 30.9  Nombres 16.33  Psaumes 88.10-88.11  
 19  Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto kweli yako. 
Deutéronome 6.7  Deutéronome 4.9  Psaumes 78.3-78.6  Deutéronome 11.19  Exode 12.26-12.27  
 20  Bwana yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa Bwana. 
Psaumes 27.5-27.6  Psaumes 116.17-116.19  Psaumes 150.4  Habakuk 3.19  Psaumes 116.2  
 21  Maana Isaya amesema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona. 
Marc 7.33  2 Rois 20.7-20.8  Jean 9.6  
 22  Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionyesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa Bwana? 
Psaumes 84.10-84.12  Psaumes 84.1-84.2  Jean 5.14  Psaumes 118.18-118.19  Psaumes 122.1