Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 7.8
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye.Psaumes 31.15 Habakuk 3.1 Esaïe 50.10 Psaumes 13.5 Psaumes 3.7
2 Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya.Psaumes 50.22 Esaïe 38.13 Psaumes 22.13 Psaumes 17.12 Job 10.7
3 Bwana, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu,1 Samuel 24.11 Psaumes 59.3 2 Samuel 16.7-16.8 1 Samuel 26.18-26.19 Job 11.14
4 Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)1 Samuel 24.7 Psaumes 109.5 Psaumes 55.20 1 Samuel 24.10-24.15 1 Samuel 26.24
5 Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.Jérémie 17.13 Esaïe 63.3 Psaumes 60.12 Job 31.5-31.10 Job 40.12-40.13
6 Bwana uondoke kwa hasira yako; Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.Psaumes 44.23 Psaumes 35.23 Psaumes 3.7 Esaïe 33.10 Psaumes 12.5
7 Kusanyiko la mataifa na likuzunguke, Na juu yake uketi utawale.Apocalypse 18.20 Psaumes 58.10-58.11 Psaumes 138.6 Psaumes 48.11 Psaumes 93.4
8 Bwana atawaamua mataifa, Bwana, unihukumu mimi, Kwa kadiri ya haki yangu, Sawasawa na unyofu nilio nao.Psaumes 96.13 Romains 14.10-14.12 Psaumes 98.9 2 Corinthiens 1.12 Psaumes 43.1
9 Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na viuno Ndiye Mungu aliye mwenye haki.Apocalypse 2.23 Jérémie 11.20 Psaumes 37.23 1 Chroniques 28.9 1 Samuel 16.7
10 Ngao yangu ina Mungu, Awaokoaye wanyofu wa moyo.Psaumes 125.4 Proverbes 11.20 Psaumes 18.1-18.2 Genèse 15.1 Psaumes 112.2
11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku.Nahum 1.2 Psaumes 94.15 Nahum 1.6 Psaumes 50.6 Psaumes 7.8
12 Mtu asiporejea ataunoa upanga wake; Ameupinda uta wake na kuuweka tayari;Deutéronome 32.41 Psaumes 85.4 Actes 3.19 Ezéchiel 21.23 Matthieu 3.10
13 Naye amemtengenezea silaha za kufisha, Akifanya mishale yake kuwa ya moto.Psaumes 45.5 Psaumes 64.3 Deutéronome 32.23 Lamentations 3.12-3.13 Psaumes 11.2
14 Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.Jacques 1.15 Job 15.35 Esaïe 33.11 Esaïe 59.4-59.5 Job 15.20
15 Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoifanya!Job 4.8 Psaumes 119.85 Psaumes 141.10 Proverbes 26.27 Psaumes 35.7-35.8
16 Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini.Esther 9.25 1 Rois 2.32 Psaumes 37.12-37.13 Psaumes 36.4 Psaumes 36.12
17 Nitamshukuru Bwana kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu.Psaumes 9.2 Psaumes 71.15-71.16 Daniel 4.17 Daniel 4.25 Daniel 4.34

Cette Bible est dans le domaine public.