Prière du roi qui cherche un refuge
 1  Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. 
Psaumes 4.1  Philippiens 4.6  Psaumes 55.1-55.2  Psaumes 5.1-5.3  Psaumes 6.1  
 2  Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. 
Psaumes 77.3  Psaumes 18.2  Deutéronome 4.29  Psaumes 62.6  Psaumes 62.2  
 3  Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. 
Proverbes 18.10  Psaumes 116.2  2 Corinthiens 1.10  Psaumes 140.7  Psaumes 62.7  
 4  Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako 
Psaumes 17.8  Psaumes 91.4  Psaumes 27.4  Psaumes 23.6  Psaumes 15.1  
 5  Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako. 
Psaumes 56.12  Psaumes 66.19  Psaumes 115.13  Psaumes 86.11  Psaumes 16.5-16.6  
 6  Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. 
Psaumes 21.4  Psaumes 21.6  Esaïe 53.10  Psaumes 89.36-89.37  Psaumes 72.15-72.17  
 7  Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi. 
Psaumes 40.11  Psaumes 41.12  Psaumes 57.3  Esaïe 9.6-9.7  Michée 7.20  
 8  Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku. 
Psaumes 65.1  Psaumes 145.1-145.2  Psaumes 66.13-66.16  Psaumes 146.2  Psaumes 71.22