Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 57.2
Bible en Swahili de l’est


1 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hata misiba hii itakapopita.Psaumes 91.4 Esaïe 26.20 Psaumes 63.7 Psaumes 36.7 Ruth 2.12
2 Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.Psaumes 138.8 Philippiens 1.6 Esaïe 26.12 Hébreux 13.21 Psaumes 56.2
3 Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa, Atukanapo yule atakaye kunimeza. Mungu atazipeleka Fadhili zake na kweli yakePsaumes 40.11 Psaumes 43.3 Psaumes 56.1-56.2 Actes 12.11 Job 31.31
4 Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.Psaumes 58.6 Psaumes 55.21 Proverbes 12.18 Psaumes 35.17 Proverbes 30.14
5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.Habakuk 2.14 Esaïe 6.3 Psaumes 72.19 Psaumes 57.11 Nombres 14.21
6 Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nafsi yangu imeinama; Wamechimba shimo mbele yangu; Wametumbukia ndani yake!Psaumes 145.14 Psaumes 140.5 Psaumes 35.7-35.8 Psaumes 143.4 Proverbes 29.5
7 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Moyo wangu u thabiti. Nitaimba, nitaimba zaburi,Psaumes 112.7 Psaumes 108.1-108.5 Esaïe 24.15 Psaumes 34.4 Ephésiens 5.20
8 Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.Psaumes 16.9 Psaumes 30.12 Juges 5.12 Esaïe 52.9 Psaumes 150.3
9 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.Psaumes 138.1 Psaumes 96.3 Psaumes 2.1 Psaumes 22.22-22.23 Psaumes 18.49
10 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni.Psaumes 103.11 Psaumes 36.5 Psaumes 108.4 Psaumes 71.19 Esaïe 54.7-54.10
11 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.Psaumes 57.5 Apocalypse 15.3-15.4 Psaumes 8.1 Psaumes 8.9

Cette Bible est dans le domaine public.