Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 55.4
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, uisikilize sala yangu, Wala usijifiche nikuombapo rehema.Psaumes 61.1 Psaumes 80.4 Psaumes 80.1 Psaumes 27.9 Psaumes 28.1
2 Unisikilize na kunijibu, Nimetanga-tanga nikilalama na kuugua.Esaïe 38.14 Esaïe 59.11 Psaumes 77.3 Psaumes 64.1 Psaumes 38.6
3 Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi.2 Samuel 16.7-16.8 Psaumes 73.8 Psaumes 71.11 2 Samuel 19.19 Psaumes 12.5
4 Moyo wangu unaumia ndani yangu, Na hofu za mauti zimeniangukia.Psaumes 116.3 Psaumes 18.4-18.5 Marc 14.33-14.34 Esaïe 38.10-38.13 Psaumes 88.3
5 Hofu na tetemeko limenijia, Na hofu kubwa imenifunikiza.Psaumes 119.120 Job 21.6 Job 6.4 Psaumes 88.15-88.16 Psaumes 42.6
6 Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningerukia mbali na kustarehe.Apocalypse 12.14 Psaumes 139.9 Psaumes 11.1
7 Ningekwenda zangu mbali, Ningetua jangwani.Jérémie 9.2 Jérémie 37.12 1 Samuel 27.1 Proverbes 6.4-6.5 2 Samuel 15.14
8 Ningefanya haraka kuzikimbia Dhoruba na tufani.Esaïe 4.6 Matthieu 7.25-7.27 Esaïe 17.12-17.13 Psaumes 18.4
9 Ee Bwana, uwaangamize, uzichafue ndimi zao, Maana nimeona dhuluma na fitina katika mji.Jérémie 6.7 2 Samuel 15.31 2 Samuel 17.1-17.14 Genèse 11.7-11.9 Matthieu 23.37-23.38
10 Mchana na usiku huzunguka kutani mwake; Uovu na taabu zimo ndani yake;Psaumes 59.14-59.15 Esaïe 59.6-59.15 Jean 18.3 Jean 18.28 2 Samuel 16.21-16.22
11 Tamaa mbaya zimo ndani yake; Dhuluma na hila haziondoki mitaani mwake.Psaumes 10.7 Jérémie 5.26-5.27 Ezéchiel 22.1-22.12 Jérémie 9.3-9.5 Psaumes 109.2-109.3
12 Kwa maana aliyetukana si adui; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione.Psaumes 41.9 Psaumes 35.26 Matthieu 26.21-26.23 Jean 13.18 Jean 18.2-18.3
13 Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.2 Samuel 15.12 Psaumes 41.9 Jérémie 9.4 Michée 7.5 2 Samuel 16.23
14 Tulipeana shauri tamu; na kutembea Nyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.Psaumes 42.4 Psaumes 122.1 Esaïe 2.3 Ezéchiel 33.31
15 Mauti na iwapate kwa ghafula, Na washuke kuzimu wangali hai, Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.Matthieu 26.24 Psaumes 69.22-69.28 2 Samuel 17.23 2 Samuel 18.9 Psaumes 59.13
16 Nami nitamwita Mungu, Na Bwana ataniokoa;Luc 6.11-6.12 Psaumes 50.15 Psaumes 109.4 Psaumes 73.28 Psaumes 91.15
17 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.Actes 3.1 Ephésiens 6.18 Psaumes 141.2 1 Thessaloniciens 5.17 Actes 10.3
18 Ameiokoa nafsi yangu iwe salama, asinikaribie mtu, Maana walioshindana nami walikuwa wengi.1 Jean 4.4 Matthieu 26.53 Psaumes 57.3 Psaumes 118.10-118.12 2 Rois 6.16
19 Mungu atasikia na kuwajibu; Ndiye Yeye akaaye tangu milele. Mageuzi ya mambo hayawapati hao, Kwa hiyo hawamchi Mungu.Deutéronome 33.27 Psaumes 90.1-90.2 Psaumes 65.5 1 Thessaloniciens 2.15-2.16 Psaumes 73.5-73.6
20 Amenyosha mkono awadhuru waliopatana naye, Amelihalifu agano lake.Psaumes 89.34 Psaumes 7.4 Actes 12.1 1 Samuel 22.17 2 Samuel 5.3
21 Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Bali hayo ni panga wazi.Psaumes 28.3 Psaumes 57.4 Proverbes 5.3-5.4 Proverbes 26.24-26.26 Psaumes 62.4
22 Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.Psaumes 37.5 1 Pierre 5.7 Matthieu 6.25 Philippiens 4.6-4.7 Psaumes 37.24
23 Nawe, Ee Mungu, utawatelemsha, Walifikilie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.Proverbes 10.27 Job 15.32 Psaumes 5.6 Esaïe 38.17 Psaumes 58.9

Cette Bible est dans le domaine public.