La beauté de Sion
 1  Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu. 
Michée 4.1  Zacharie 8.3  Psaumes 46.4  Psaumes 145.3  Esaïe 2.2-2.3  
 2  Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu. 
Matthieu 5.35  Psaumes 50.2  Lamentations 2.15  Esaïe 14.13  Ezéchiel 20.6  
 3  Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome. 
Esaïe 4.5-4.6  2 Chroniques 14.9-14.15  Zacharie 2.4-2.5  Psaumes 46.7  2 Chroniques 20.1-20.37  
 4  Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja. 
Apocalypse 17.12-17.14  2 Samuel 10.6-10.19  Esaïe 7.1  Esaïe 10.8  Psaumes 83.2-83.8  
 5  Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia. 
2 Rois 19.35-19.37  Exode 14.25  2 Rois 7.6-7.7  
 6  Papo hapo tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye. 
Osée 13.13  Exode 15.15-15.16  Esaïe 21.3  Daniel 5.6  Esaïe 13.6-13.8  
 7  Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za Tarshishi. 
Jérémie 18.17  1 Rois 22.48  Ezéchiel 27.25-27.26  1 Rois 10.22  Esaïe 2.16  
 8  Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya imara hata milele. 
Psaumes 87.5  Esaïe 2.2  Michée 4.1  Matthieu 16.18  Psaumes 48.1-48.2  
 9  Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako. 
Psaumes 26.3  Psaumes 40.10  Psaumes 104.34  Luc 22.19-22.20  Psaumes 105.5-105.6  
 10  Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia. Mkono wako wa kuume umejaa haki; 
Deutéronome 28.58  Malachie 1.11  Josué 7.9  Malachie 1.14  Psaumes 113.3  
 11  Na ufurahi mlima Sayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu zako. 
Psaumes 97.8  Apocalypse 16.5-16.7  Apocalypse 15.4  Cantique 1.5  Cantique 5.16  
 12  Tembeeni katika Sayuni, Uzungukeni mji, Ihesabuni minara yake, 
Esaïe 33.18-33.20  Matthieu 24.1-24.2  Néhémie 12.31-12.40  
 13  Tieni moyoni boma zake, Yafikirini majumba yake, Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja. 
Psaumes 122.7  Joël 1.3  Psaumes 78.4-78.6  Amos 9.11  Deutéronome 11.19  
 14  Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza. 
Psaumes 23.3-23.4  Psaumes 73.24  Esaïe 58.11  Psaumes 25.9  Psaumes 73.26