Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 31.4
Bible en Swahili de l’est


1 Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye,Psaumes 25.2 Romains 10.11 Psaumes 143.1 Psaumes 71.1-71.3 Romains 5.5
2 Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.Psaumes 102.2 Psaumes 86.1 Psaumes 71.2-71.3 Deutéronome 32.31 Psaumes 143.7
3 Ndiwe genge langu na ngome yangu; Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge.Josué 7.9 Psaumes 25.9 Psaumes 18.2 Psaumes 25.11 Néhémie 9.19
4 Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu.Psaumes 25.15 2 Timothée 2.26 2 Corinthiens 12.9 Psaumes 140.5 Psaumes 124.7
5 Mikononi mwako naiweka roho yangu; Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli.Luc 23.46 Actes 7.59 Deutéronome 32.4 Psaumes 71.23 Tite 2.14
6 Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumaini Bwana.Psaumes 26.5 Jonas 2.8 1 Corinthiens 10.20 Jérémie 10.8 Romains 1.21
7 Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni,Esaïe 63.9 Psaumes 119.153 Esaïe 49.13 Psaumes 1.6 Néhémie 9.32
8 Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi.Deutéronome 32.30 Job 36.16 1 Samuel 24.18 Esaïe 19.4 Job 16.11
9 Ee Bwana, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu.Psaumes 6.7 Psaumes 88.9 Psaumes 6.1-6.2 Psaumes 107.10 Psaumes 44.25
10 Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni, Na miaka yangu kwa kuugua. Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imekauka.Psaumes 38.3 Psaumes 32.3-32.4 Psaumes 78.33 Romains 9.2 Psaumes 88.15
11 Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Walioniona njiani walinikimbia.Psaumes 38.11 Psaumes 88.8 Esaïe 49.7 Job 19.13-19.14 Psaumes 41.8-41.9
12 Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa; Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.Psaumes 88.4-88.5 Esaïe 30.14 Esaïe 38.11-38.12 Psaumes 2.9 Apocalypse 2.27
13 Maana nimesikia masingizio ya wengi; Hofu ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walifanya hila wauondoe uhai wangu.Matthieu 27.1 Jérémie 20.10 Lamentations 2.22 2 Samuel 17.1-17.4 Psaumes 55.10
14 Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.Psaumes 43.5 Psaumes 56.3-56.4 Psaumes 71.22 Psaumes 18.2 Matthieu 26.42
15 Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.Job 24.1 Jean 7.6 2 Samuel 7.12 Actes 1.7 1 Samuel 26.10
16 Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.Psaumes 4.6 Psaumes 80.3 Psaumes 6.4 Ephésiens 2.4-2.7 Psaumes 67.1
17 Ee Bwana, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.Psaumes 25.2-25.3 Psaumes 115.17 Esaïe 41.11-41.12 Psaumes 71.24 Psaumes 69.6-69.7
18 Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.Psaumes 94.4 Jude 1.15 1 Samuel 2.3 Apocalypse 21.8 Jean 8.48
19 Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!1 Corinthiens 2.9 Esaïe 64.4 1 Pierre 1.4-1.5 Lamentations 3.23-3.25 Jacques 2.5
20 Utawasitiri na fitina za watu Katika sitara ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na mashindano ya ndimi.Psaumes 27.5 Psaumes 32.7 Job 5.21 Psaumes 10.2 Psaumes 86.14
21 Bwana ahimidiwe; kwa maana amenitendea Fadhili za ajabu katika mji wenye boma.Psaumes 17.7 Jérémie 1.18 1 Samuel 23.7-23.13 Psaumes 98.1 1 Pierre 2.9
22 Nami nalisema kwa haraka yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya dua yangu Wakati nilipokulilia.Psaumes 116.11 Jonas 2.4 2 Chroniques 33.11-33.13 1 Samuel 27.1 Psaumes 6.9
23 Mpendeni Bwana, Ninyi nyote mlio watauwa wake. Bwana huwahifadhi waaminifu, Humlipa atendaye kiburi malipo tele.Psaumes 97.10 Psaumes 30.4 Psaumes 94.2 Psaumes 34.9 Psaumes 145.20
24 Iweni hodari, mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja Bwana.Psaumes 27.14 Hébreux 12.12-12.13 Romains 15.12-15.13 Colossiens 1.11 Luc 22.31-22.32

Cette Bible est dans le domaine public.