1  Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye, 
Psaumes 25.2  Romains 10.11  Psaumes 143.1  Psaumes 71.1-71.3  Daniel 9.16  
 2  Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Nyumba yenye maboma ya kuniokoa. 
Psaumes 102.2  Psaumes 86.1  Psaumes 71.2-71.3  Deutéronome 32.31  Job 7.21  
 3  Ndiwe genge langu na ngome yangu; Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge. 
Psaumes 25.9  Psaumes 18.2  Psaumes 25.11  Néhémie 9.19  Luc 1.79  
 4  Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu. 
Psaumes 25.15  2 Corinthiens 12.9  Psaumes 140.5  Psaumes 124.7  Proverbes 29.5  
 5  Mikononi mwako naiweka roho yangu; Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli. 
Luc 23.46  Actes 7.59  Deutéronome 32.4  Psaumes 71.23  Tite 2.14  
 6  Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumaini Bwana. 
Psaumes 26.5  Jonas 2.8  1 Corinthiens 10.20  Romains 1.21  1 Chroniques 16.28-16.29  
 7  Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni, 
Esaïe 63.9  Psaumes 119.153  Esaïe 49.13  Psaumes 1.6  Psaumes 142.3  
 8  Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi. 
Deutéronome 32.30  Job 36.16  Esaïe 19.4  Job 16.11  1 Samuel 26.8  
 9  Ee Bwana, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu. 
Psaumes 6.7  Psaumes 88.9  Psaumes 107.10  Psaumes 44.25  Psaumes 38.1-38.10  
 10  Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni, Na miaka yangu kwa kuugua. Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imekauka. 
Psaumes 38.3  Psaumes 32.3-32.4  Romains 9.2  Psaumes 88.15  Job 3.24  
 11  Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Walioniona njiani walinikimbia. 
Psaumes 38.11  Psaumes 88.8  Esaïe 49.7  Job 19.13-19.14  Psaumes 41.8-41.9  
 12  Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa; Nimekuwa kama chombo kilichovunjika. 
Psaumes 88.4-88.5  Esaïe 30.14  Psaumes 2.9  Apocalypse 2.27  Psaumes 119.83  
 13  Maana nimesikia masingizio ya wengi; Hofu ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walifanya hila wauondoe uhai wangu. 
Matthieu 27.1  Jérémie 20.10  Lamentations 2.22  2 Samuel 17.1-17.4  Psaumes 55.10  
 14  Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu. 
Psaumes 43.5  Psaumes 56.3-56.4  Psaumes 18.2  Matthieu 26.42  Matthieu 26.39  
 15  Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. 
Job 24.1  Jean 7.6  2 Samuel 7.12  Actes 1.7  Actes 27.24  
 16  Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. 
Psaumes 4.6  Psaumes 80.3  Psaumes 6.4  Psaumes 67.1  Psaumes 80.19  
 17  Ee Bwana, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni. 
Psaumes 25.2-25.3  Psaumes 115.17  Esaïe 41.11-41.12  Psaumes 69.6-69.7  Psaumes 94.17  
 18  Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau. 
Psaumes 94.4  Jude 1.15  1 Samuel 2.3  Jean 8.48  Psaumes 64.3-64.4  
 19  Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu! 
1 Corinthiens 2.9  Esaïe 64.4  1 Pierre 1.4-1.5  Lamentations 3.23-3.25  Jacques 2.5  
 20  Utawasitiri na fitina za watu Katika sitara ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na mashindano ya ndimi. 
Psaumes 27.5  Psaumes 32.7  Job 5.21  Psaumes 86.14  Jacques 3.14-3.16  
 21  Bwana ahimidiwe; kwa maana amenitendea Fadhili za ajabu katika mji wenye boma. 
Psaumes 17.7  1 Samuel 23.7-23.13  Psaumes 98.1  1 Pierre 2.9  Psaumes 118.23  
 22  Nami nalisema kwa haraka yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya dua yangu Wakati nilipokulilia. 
Psaumes 116.11  Jonas 2.4  1 Samuel 27.1  Psaumes 6.9  Psaumes 88.16  
 23  Mpendeni Bwana, Ninyi nyote mlio watauwa wake. Bwana huwahifadhi waaminifu, Humlipa atendaye kiburi malipo tele. 
Psaumes 97.10  Psaumes 30.4  Psaumes 94.2  Psaumes 34.9  1 Samuel 2.9  
 24  Iweni hodari, mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja Bwana. 
Psaumes 27.14  Hébreux 12.12-12.13  Romains 15.12-15.13  Colossiens 1.11  Luc 22.31-22.32