Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 28.7
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, nitakuita Wewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.Psaumes 83.1 Psaumes 18.2 Psaumes 143.7 Psaumes 35.22 Psaumes 88.4-88.6
2 Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo, Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.Psaumes 138.2 Psaumes 141.2 Psaumes 5.7 1 Timothée 2.8 Psaumes 134.2
3 Usinikokote pamoja na wasio haki, Wala pamoja na watenda maovu. Wawaambiao jirani zao maneno ya amani, Lakini mioyoni mwao mna madhara.Psaumes 12.2 Psaumes 55.21 Psaumes 26.9 Psaumes 62.4 Matthieu 25.41
4 Uwape sawasawa na vitendo vyao, Na kwa kadiri ya ubaya wa kufanya kwao, Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao, Uwalipe stahili zao.2 Timothée 4.14 Apocalypse 18.6 Psaumes 62.12 Psaumes 109.17-109.21 Psaumes 2.1-2.5
5 Maana hawazifahamu kazi za Bwana, Wala matendo ya mikono yake. Atawavunja wala hatawajenga;Esaïe 5.12 Esaïe 45.18 Nombres 23.23 Esaïe 40.26 Psaumes 10.5
6 Na ahimidiwe Bwana. Maana ameisikia sauti ya dua yangu;Psaumes 66.19-66.20 Psaumes 116.1-116.2 Psaumes 31.21-31.22 Psaumes 69.33-69.34 Psaumes 107.19-107.22
7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.Psaumes 13.5 Esaïe 61.10 Psaumes 30.11-30.12 Psaumes 69.30 Psaumes 56.3-56.4
8 Bwana ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.Psaumes 20.6 1 Samuel 16.13 Esaïe 61.1 Psaumes 140.7 Psaumes 2.2
9 Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge, uwachukue milele.Esaïe 40.11 Deutéronome 9.29 Psaumes 78.71 1 Rois 8.51 Esdras 1.4

Cette Bible est dans le domaine public.