Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 148.6
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Msifuni Bwana kutoka mbinguni; Msifuni katika mahali palipo juu.Luc 2.13-2.14 Psaumes 69.34 Apocalypse 19.1-19.6 Psaumes 89.5 Esaïe 49.13
2 Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote.Psaumes 103.20-103.21 Apocalypse 5.11-5.13 Esaïe 6.2-6.4 Job 38.7 Genèse 2.1
3 Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga.Psaumes 19.1-19.6 Genèse 8.22 Jérémie 33.20 Psaumes 89.36-89.37 Deutéronome 4.19
4 Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.Genèse 1.7 1 Rois 8.27 Néhémie 9.6 Psaumes 68.33 Genèse 7.11
5 Na vilisifu jina la Bwana, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.Psaumes 33.6-33.9 Genèse 1.6 Jérémie 10.11-10.13 Apocalypse 4.11 Amos 9.6
6 Amevithibitisha hata milele na milele, Ametoa amri wala haitapita.Jérémie 33.25 Job 38.33 Jérémie 31.35-31.36 Psaumes 89.37 Psaumes 119.90-119.91
7 Msifuni Bwana kutoka nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote.Genèse 1.21 Psaumes 74.13-74.14 Esaïe 27.1 Psaumes 104.25-104.26 Job 41.1-41.34
8 Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba ulitendao neno lake.Psaumes 147.15-147.18 Exode 10.13 Psaumes 103.20 Psaumes 18.12 Lévitique 10.2
9 Milima na vilima vyote, Miti yenye matunda na mierezi yote.Esaïe 44.23 Esaïe 49.13 Psaumes 98.7-98.9 Psaumes 97.4-97.5 Psaumes 96.11-96.13
10 Hayawani, na wanyama wafugwao, Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.Genèse 7.14 Psaumes 50.10-50.11 Genèse 1.20-1.25 Psaumes 150.6 Ezéchiel 17.23
11 Wafalme wa dunia, na watu wote, Wakuu, na makadhi wote wa dunia.Psaumes 102.15 Proverbes 8.15-8.16 Psaumes 68.31-68.32 Psaumes 138.4-138.5 Apocalypse 21.24
12 Vijana waume, na wanawali, Wazee, na watoto;Tite 2.4-2.6 Psaumes 8.2 Luc 19.37 Psaumes 68.25 Matthieu 21.15-21.16
13 Na walisifu jina la Bwana, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.Psaumes 113.4 Psaumes 8.1 Esaïe 12.4 Zacharie 9.17 Psaumes 57.6
14 Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.Ephésiens 2.17 1 Samuel 2.1 Psaumes 75.10 Deutéronome 4.7 Apocalypse 5.8-5.14

Cette Bible est dans le domaine public.