Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 8.1
Bible en Swahili de l’est


1 Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; 2 Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi. 3 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; 4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. 7 Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini. 9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

Cette Bible est dans le domaine public.